MASHEHA WATAKIWA KUTOA ELIMU KWA JAMII JUU UWEPO WA BARAZA LA KUMUWAKILISHA MTUMIAJI crc]
Masheha wa shehia mbali mbali kutoka wilaya ya Micheweni wametakiwa kuwa mabalozi wazuri wa kuifikisha elimu juu ya kulijua na kulitumia baraza la kumuwakilisha mtumiaji wa huduma za maji na nishati katika shehia zao ili Wananchi waweze kufikisha kero zao katika baraza hilo.
Hayo yameelezwa
na Kaimu katibu Tawala wilaya ya Micheweni Kai Shaame Kai wakati akifungua
mafunzo ya siku moja juu ya kulijua Baraza la kumuwakilisha mtumiaji wa huduma
za maji a Niashati kwa masheha wa wilaya hiyo huko Micheweni Mkoa wa kaskazini
Pemba.
Amesema Masheha wananafasi kubwa ya kuwafahamisha wanajamii juu ya matumizi ya huduma za maji na Nishati pamoja na kuwafahamisha uwepo wa baraza hilo kwa lengo la kufikisha changamoto zao .
Akizungumzia
juu ya uwepo wa Baraza hilo katibu mtendaji wa baraza la kumuakilisha mtumiaji wa huduma za maji na
Nishati [CRC ] Hadia Abdurahman Othman amesema lengo la kuwanzishwa chombo
hicho ni kuwatetea watumiaji wa huduma hizo
katika kutatua kero zao na kuzifanya huduma za maji na Nishati kuwa bora
kwaZanzibar.
Amesema
Serikali kwa kuwajali wananchi wake imeamua kwa makusudi kuanzisha chombo hicho
ili kutetea malalamiko ya wananchi jambo ambalo litasaidia upatikanaji wa
huduma za kijamii kwa urahisi.
Amesema
Vijiji vingi vimekua vikilalamikia juu
ya ukosefu wa huduma za maji safi pamoja na umeme, hivyo masheha mnajukumu
kubwa la kushirikiana na CRC ili
kuhakikisha shehiya zenu zinapata huduma hizo.
Akiwasilisha
mada juu ya haki na wajibu wa mtumiaji mtendaji kutoka baraza la kumuakilisha
mtumiaji [ CRC] Khamis Ame Mnubi amesema lengo la mkutano huo kwa masheha ni
kutoa elimu kwa jamii kufahamu kwamba, upatikanaji wa huduma hizo ni haki yao
ya msingi, hivyo wasibaki kimya bali watoe malalamiko wakati wanapozikosa na
kuona zinapatiwa ufumbuzi.
Wakitoa
ufafanuzi wawakilishi kutoka shirika la Umeme na Mamlaka ya maji wilaya ya micheweni Ali Rajabu na Suleiman Salim Shajaki
wamesema kwa sasa wamejipanga vyema ili kuona kero za wananchi zimeondoka.
Comments
Post a Comment