MAULID KHAMIS KASSIM NI MFANYABIASHARA MLEMAVU AOMBA MSAADA KWA WASAMARIA WEMA ILI AKUZE BIASHARA YAKE
Maulid mwenye
familia ya watoto watano anasema kuwa aliamua kuanzisha biashara zake ndogo ndogo
mara baada ya kumaliza masomo yake ya lazima ya kidato cha 2 katika Skuli ya Sekondari
Wawi kwa kuanzia na biashara ya malai, juice na biskuti za watoto kwa mtaji wa
shilingi elfu arobaini.
Kwa sasa
Maulid anafanya biashara ya nguo za watoto huko Mjini Chake Chake ambapo alianza na mtaji wa shilingi laki mbili na hadi sasa anasema mtaji wake unaweza kufika milioni
moja.
Ameeleza
kuwa licha ya ulemavu wake alionao aliamua kujiajiri ili aepukane na omba omba,
na utegemezi kwa watu wengine, huku akijua kuwa yeye anahitaji kuwa na mahitaji
kama binadamu wote ikiwemo kuwa na mke na watoto.
‘’Niliamua nijiajiri mwenyewe ili niepukane na
kuomba jambo ambalo litaniepusha na udhalilishaji, Alieleza Maulid’’.
Maulid
alisema kutokana na biashara yake
anaendesha familia yake mwenyewe, na anasomesha
watoto wake ambapo mtoto wa
mwanzo anasoma darasa la Tatu, wa pili anasoma darasa la kwanza katika Skuli ya
Michakaini na watatu anasoma Chekechea Machomane.
‘’Naendesha
familia yangu mwenyewe, si mtegemei mtu,
wala siombi, na watoto wangu wote wanasoma Shule pamoja na Madrasa,
Alisema Maulid.’’
Hata hivyo
ameleza kuwa familia yake iko pamoja nae haija mtenga, wanamshirikisha katika
masuala mbali ya kifamilia yanapotokezea na pia husaidia baadhi ya
mahitaji ya nyumbani kwake.
Akitaja
changamoto ambazo anakumbana nazo ni kukosa fursa ya kupata mikopo isiyo na riba
jambo ambalo linamkosesha kuendesha biashara zake ipasavo.
‘’Sjapata
msaada wowote wala sjui wapi pakwenda
nikaweza kusaidiwa, Alisema Maulid.’’
Hivyo
amesema endapo atapatiwa mkopo wa shilling Milioni mbili ana uwezo wa
kuzifanyia biashara na kuzirejesha.
Aidha ameitaka
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoa punguzo maalum la ulipaji wa kodi za
biashara kwa watu wenye ulemavu, jambo ambalo litawafanya waendeleze biashara
zao.
‘’Kodi
tunayolipa ni kubwa hatuiwezi kulingana na biashara zetu ni ndogo hivyo
tunaiomba serikali ituangalie na sisi Walemavu’’, Alisema Maulid.
Kwa upande
mwengine aliwashauri watu wenye ulemavu wenzake ambao wanajiweza wafanye kazi ili wasiwe wa tegemezi katika
Jamii na kuweza kujipatia riziki
zao za halali.
Comments
Post a Comment