RASIMU YA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MAFUTA NA GESI ASILIA YA ZANZIBAR ITAWEZA KUSAIDIA KUKUZA UCHUMI WA NCHI.
SALIM HAMAD,PEMBA
WADAU na Watendaji wa taasisi mbali mbali za Umma Kisiwani
Pemba,wamesema iwapo rasimu ya marekebisho ya Sheria za mafuta na Gesi asilia
ya Zanzibar itaweza kusadia kukuza maslahi ya Umma.
Wakizingumza katika mkutano wa kujadili rasimu ya marekebisho
ya Sheri za mafuta na gesi Asilia ya mwaka 2016 uliofanyika Gombani Chake chake
Pemba wamesema itasadia kutatua changamoto kwa baadhi ya vifungu ambavyo
vilikuwa vinajitokeza hapoawali.
Akiwasilisha mada katika Mkutano huo Mwanasheria kutoka
taasisiya ZPRA Omari Sururu Khalfani amefahamisha Vipengele vilivyofanyiwa
marekebisho ikiwemo mkanganyiko watafsiri.
Alisema tayari kwenye maeneo hayo walibaini kuna mapungufu na
kuweza kuyafanyia marekebisho kuona mapungufu hayo yanaondoka.
Afisa mdhamini Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi Kisiwani
Pemba,Dr Salum Mohd Hamza alisema lengo kuu la kuwakutanisha wadau mbali mbali
ni kutafuta maoni juu ya marekebisho ya sheria za mafuta na gesi asilia.
‘’Tumefanya mkutano na wadau wa taasisi mbali mbali za umma
ikiwa lengo ni kutafuta maoni ya wananchi juu ya rasimu ya marekebisho ya
sheria za mafuta na gesi asilia na tukafanikiwa kupata michango yao’’alisema.
Alisema wadau waliweza kuikubali na kuchangia baadhi
ya Vipengele ambavyo vinahitaji kufanyiwa maboresho zaidi kabla ya kupitishwa rasimu
ya Sheria ya Mafuta na Gesi Visiwani Zanzibar.
.
Comments
Post a Comment