MAMA MWENYE WATOTO SITA WALEMAVU WA VIUNGO AOMBA MSAADA ILI AWEZE KUENDESHA MAISHA YA WATOTO WAKE



JAMII imetakiwa kuwajali na kuwasaidia kupata mahitaji muhimu ikiwemo elimu, afya na mavazi Watoto wenye ulemavu wa akili  ili waondokane na dhana ya unyanyapaa .

 Ushauri huo umetolewa na familia ya watoto wenye ulemavu wa viungo shehia ya Kinyasini Wilaya ya Wete Kisiwani Pemba baada ya watoto wao kushindwa kuendelea na masomo kutokana na ukali ya maisha.

 Mama mazazi wa Watoto hao Mariam Ali Kombo amesema anashindwa kufanyakazi za maendeleo kutokana na changamoto zinazowakabili ikiwemo kufuata huduma ya maji.

 “Nashindwa hata kufanya kazi kwa kuwalinda na kuwahudumia Watoto wangu, hivyo naomba yoyote mwenye uwezo anisaidie kuniunganishia maji pamoja na sabuni za kuoshea nguo”alisema.

 Kwa upande wake Afisa  Idara ya watu Ulemavu Wilaya ya Wete Mohammed Mgau Said aliitaka jamii kushajishina na katika kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu kwani wanayofursa ya kupatiwa mahitaji ya msingi ikiwemo suala la elimu na kushirikishwa.

 Amesema Pamoja na Watoto hawa kuwa na ulemavu wa akili , lakini wanahitaji kushirikishwa katika kazi  mbali mbali Pamoja na kupatiwa elimu.

 “Watoto hawa wanahitaji kupatiwa elimu na kushirikishwa Pamoja na kwamba wanaulemavu wa akili”alieleza.

 Aidha Mohammed amesema ni wajibu wa kila mzazi kuhakikisha Watoto wote wanapatiwa mahitaji ya masingi bila ya misingi ya ubaguzi.



 

 


Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.