WAFANYA KAZI WA KITENGO CHA ELIMU YA AFYA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA JAMII KUTOA ELIMU ILI KUTOKOMEZA UGONJWA WA KIPINDU PINDU



 Wafanyakazi wa kitengo cha kinga na elimu ya afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wametakiwa

kushirikiana kwa pamoja katika kuendeleza kinga ili kuondosha kabisa ugonjwa wa kipindupindu kisiwani

Zanzibar.

Akizungumza mratibu mkuu wa elimu ya afya Zanzibar Halima ali khamis wakati wa uwasilisho wa tafiti

fupi iliyofanywa na kitengo hicho amesema matarajio ya serikali kupitia KOICA ni kumaliza maradhi hayo

ifikapo 2027.

Amengeza kuwa kutokana na mtarajio hayo zipo mbinu tofauti zinazochukuliwa na serikali kupitia

mpango wa kupambana na kumaliza kipindupindu ikiwemo uhamasishaji wa uchimbaji wa vyoo na

kuvitumia, upigaji wa chanjo na matumizi sahihi wa maji safi na salama mijini na vijijini.

Kwa niaba ya afisi ya mufti pemba sheikh said ahmad mohammed amesema , hata dini imesisitiza juu ya

kujikinga na maradhi mbalimbali hivyo hatuna budi kuhakikisha tunachukua hatua madhubuti katika hili.

Ameongeza kuwa wao kama afisi ya mufti watahakikisha wanatumia fursa walioipata kwa lengo la

kuhamasisha jamii juu ya kinhda vilevile ameiomba idara husika kuweza kuwafikia jamii kwa lengo la

kutoa elimu zaid.



Nao washiriki wengine waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo hayo wamesema umefika wakati wa kila

mmoja kusimama kwenye nafasi yake kuhakikisha anaisadia jamii juu ya kujikinga na majanga

mbalimbali ikiwemo kutokomeza maradhi ya kipindupindu nchini.

Mkakati wa miaka 10 umeanza 2019 hadi 2027 ambapo umeshirikisha wizara 7 tofauti na jumla ya

vipengele sa ba muhimu vimezingatiwa lengo kuu ni kupambana na kumaliza kabisa kipindupindu






Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.