umasikini wapelekea Vilabu kushindwa kusaili na uhamisho wa wachezaji Kisiwani Pemba
SALIM HAMAD,PEMBA
UKATA wa Kifedha unaovikabili Vilabu vya Madaraja mbali
mbali Kisiwani Pemba,umesababisha Dirisha la usajili na uhamisho wa wachezaji
kusuasua kutokana na baadhi ya Vilabu kushindwa kujitokeza katika Ofisi za
Shirikisho la Soka (ZFF) Kisiwani hapa.
Dirisha la Usajili na Uhamisho Visiwani Zanzibar
limefunguliwa rasmi Septemba 21 ambapo litarajiwa kufungwa Novemba 11.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Katib Msadizi wa Shirikisho la
Soka Kisiwani Pemba,Khamisi Hamad Juma alisema Zoezi la Usajili na uhamisho
limekuwa gumu msimu huu kutokana na baadhi ya Vilabu kushindwa kuchukua fomu.
Alisema moja ya sababu inayopelekea vilabu kutojitokeza
kuchuka fomu za Usajili na wachezaji wanatka kuwasajili ni kutokana na ukata wa
kifedha unaovikabili vilabu vya Pemba,jambo ambalo limepelekea zoezi hilo
kusuasua.
Alisema hadi sasa timu zilizojitokeza kuchuwa fomu kwa
upande wa Primia ni timu ya Machomane United ambayo imechukua fomu 7 na timu ya
Yoso Boys imechukua fomu 5 na timu ya Dot mond imechukua fom 4 .
Alisema kwa upande wa Vilabu vya Daraja la kwanza kanda
ya Pemba,ni timu ya Chipukizi fomu 10 New Ston Town fomu 6 Afrikana fomu 2
Mwenge fomu 3 Chake Chake Star fom 2 na Hardrock fomu 5 za ndani Zanzibar na
Fomu 7 kutoka nje ya Zanzibar ambayo ndio timu pekee iliyochukuwa fomu nyingi
kwa sasa.
‘’Dirisha la Uhamisho Visiwani Zanzibar limefungulia
tokea September 21 na linatarajiwa kufungwa rasmi November 11 saa tisa alaasiri
hivyo Vilabu vinaombwa kutumia kipindi hichi kwa kufanya mabadiliko kwenye
Vikosi vyao’’alisema Khamisi.
Hata hivyo Katibu huyo ameviomba Vilabu kujitokeza
kuitumia fursa hiyo ya usajili kuboresha timu za zao licha ya changamoto ya
ukata wa kifedha unaovikabili Vilabu vya Pemba.
Comments
Post a Comment