WASAIDIZI WA SHERIA PEMBA WAPIWA MSASA
NA FATMA HAMAD,PEMBA
AFISA mdhamini Ofisi ya Rais Katiba,
Sheria, Utumishi na Utawala Bora Halima Khamis Ali amewataka Wasaidizi wa
Sheria kuendelea kutoa Elimu kwa jamii kuhusu masuala mbali mbali ya kisheria
ili waweze kuzifahamu sharia , Haki zao pamoja wajibu wao.
Mdhamini
huyo ameyasema hao katika hafla ya ufungaji wa mafunzo ya siku tatu juu ya
kujadili mambo mbali mbali ya kimaendeleo
kwa wasaidizi wa sharia yaliofanyika Gombani Chake chake Pemba.
Alisema
Wasaidizi wa Sheria wanadhima kubwa katika kuhakikisha jamii inapata uwelewa wa
kutosha juu ya masuala mbali mbali ya kisheria pamoja na kufahamu haki zao
stahiki.
‘’Ndugu zangu Wasaidizi wa Sheria nyinyi mnajukumu kubwa la kuhakikisha Jamii inazielewa Sheria, hivyo niwaombe tu muendelee kujitoa na kujituma ili kuona Wanachi wetu wanaishi kwa amani bila migogoro alieleza,’’.
Alisema Wananchi waliowengi hawana uwelewa juu ya masula ya kisheria, hivyo ni jukumu la Wasaidizi wa Sheria kuhakikisha wanajitoa na kuipatia Elimu jamii ili iweze kuzifahamu Sheria, jambo ambalo litawafanya wawe na uthubutu wa kudai na kutetea haki zao pindi kukitokea uvunjifu wa haki hizao.
Comments
Post a Comment