WATOWA HUDUMA ZA MAMA MTOTO WATOWA YA MOYONI JUU YA HUDUMA YA M MAMA
NA FATMA HAMAD, PEMBA
WAUGUZI wanaotoa huduma za Mama na Mtoto wamesema licha ya kuanzishwa kwa huduma ya M mama ambayo imewekwa kwa lengo la kutoa usafiri wa haraka wakati ikitokezea tatizo kwa mama na mtoto, bado hauja saidia ipasavyo katika vituo hivyo.
Wakizunumza na wandishi wa habari wauguzi wa
vituo vya Afya Wesha na Pujini walisema inapotokezea tatizo la mama na mtoto
huduma za kuwahamishia Hospitali ya Wilaya inakua tatizo kwa vituo hivyo.
Amina Ali Abdi ni Muguzi Mkunga kutoka kituo cha
afya Wesha alisema mzazi anapopata tatizo akipiga simu kwa wahusika wa huduma
ya M mama, kwa ajili ya kupata usafiri inakuwa ni shida, jambo linalohatarisha maisha kwa Wazazi.
‘’Unaweza
ukapiga simu tokea asubuhi kutaka usafiri kwa Uongozi wa huduma ya M mama kwa
ajili ya kumuwahisha mgonjwa lakini haupatikani na hivyo unapopatikana haufiki kwa
wakati, na kulazimika familia ya mzazi itowe gari yenyewe ndipo tuweze
kumuhamishia Hospitali nyengine ’’alisema.
Kwa upande
wake Mkuu wa kituo hicho cha afya
Wesha Abdul nasir Hemed Said alisema mfumo wa M mama bado haujakuwa na
huduma rafiki kama ilivyotarajiwa.
Hivyo
ameiomba Serikali kuboresha huduma hiyo ya M mama ili kuona kunaondosha
matatizo yatokanayo na vifo vya mama na mtoto kama ilivyo dhamira ya Serikali.
Mratibu wa
huduma ya M mama Ofisi ya Pemba Maryam Ali Said aliwataka wahudumu wanaotoa
huduma ya Afya ya mama na mtoto kuwatumia madereva ambao walisajiliwa na wizara
ili kumuharakisha mazazi kunako husika na sio kusumbiria Ambalesi, jambo mabalo
litaepusha vifo vya mama na mtoto.
‘’Tumesha
waambia wakiona wamepata tatizo na wakipiga simu haipatikani wachukuwe madereva
waliosajiliwa ili kumuhamisha mzazi kwa haraka, na wakimaliza watowe tarifa kwa
wahusika wa M mama na kupatiwa malipo yao, wasikae nao tu wazazi,’’alieleza.
Alisema kwa sasa wameshaweka mpango mkakati wa kuhakikisha madereva wote waliosajiliwa na wizara wanapata malipo yao kwa wakati ili kuona wanafanya kazi masaa 24, jambo ambalo litaenda sambamba na dhamira ya Serikali ya kuhakikisha hakutokei vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi.
Sera ya wizara ya Afya ya Zanzibar ya mwaka 1990 ni kuhakikisha inaimarisha huduma za afya ya uzazi ya mama na mtoto, ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na vya watoto wachanga.
Comments
Post a Comment