WAZIRI KADUARA ATOA MAGIZO KWA WIZARA YA KILIMO NA YA MAJI
NA FATMA HAMAD, PEMBA
WAZIRI wa Maji na Nishati
Zanzibar Shaib Hassan Kaduara ameitaka wizara ya Kilimo kushirikiana na
Wizara ya Maji kuhakikisha wanachimba Kisima katika eneyo la Chamanangwe pamoja
na maeneo mengine, jambo ambalo litawasaidia wakulima kupata Maji na kuweza
kuzalisha mazao kwa wingi.
Waziri huyo
ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi pamoja na viongozi mbali mbali
katika hafla ya ufungaji wa siku ya
Chakula duniani huko Chamanangwe wilaya
ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba alisema Maji ni moja ya chanjo kikubwa kinachotegemewa
na wakulima wengi kwa ajili ya uzalishaji wa mazao.
Alisema maji
ndio msingi mkuu wa upatikanaji wa Chakula, hivyo ni wakati kwa wizara ya maji kuhakikisha
wanasambaza maji katika maeneo mbali mbali na wakulima waweze kuzalisha mazao mengi ili kupatikana kwa chakula cha kutosha.
‘’Ni wakati kwa
Mamlaka ya Maji pamoja na wizara ya
Kilimo kuchimba Kisima katika eneo la Chamanangwe na hata Vijijini kote
ili wakulima waweze kulima mazao ambayo yatatusaidia katika maisha
yetu,’’alisema.
Aidha
aliwaomba Wananchi kujikita zaidi katika Sekta ya kilimo ili waweze kujiajiri,
na kujipatia chakula ambacho kitasaidia
kuondokana na Njaa Kisiwani humo.
Alieleza
kuwa ukosefu wa maji unawadhibu watu zaidi ya Bilioni mbili pointi 4 Duniani kote, ambapo asilimia 10 wanaishi katika Nchi zenye
ukosefu mkubwa wa Maji.
‘’Wakulima
wadogo hasa wanawake pamoja na vijana wako hatarini zaidi kukosa maji,’’
alisema.
Katibu mkuu
wizara ya Kilimo maliasili na Mifugo Seif Shaban Mwinyi alisema kuwa bila ya
kuwepo kwa huduma ya Maji hakuwezi kupatikana kwa maendeleo, hivyo ni wakati
Serikali kuhakikisha inaimarisha huduma hiyo Vijijini kote ili kuona
kunaondokana na upungufu mkubwa wa Chakula pamoja na matunda.
Maonesho
hayo ya siku ya Chakula Duniani yaliendelea kwa muda wa siku 7 hapo katika
viwanja vya Chamanangwe ambapo ujumbe wa mwaka huu unasema Maji ni uhai, Maji
ni chakula hachwi mtu nyuma.
Comments
Post a Comment