MASHEHA WATAKIWA KUTOA ELIMU KWA JAMII KUFAHAMU ULIPAJI WA KODI YA MAJENGO
NA FATMA HAMAD,PEMBA
MKURUGENZI wa Bodi ya mapato (ZRA] kisiwani
Pemba Jmal Hassan Jamal amewataka
Masheha kuielimisha Jamii kufahamu
umuhimu wa kulipa kodi ili waweze kulipa
kodi jambo ambalo litaipatia Nchi maendeleo.
Mkurugenzi
huo ameyasema hayo wakati akizungumza na Masheha pamoja na viongozi mbali mbali
wa Serikali wa mkoa wa Kaskazini Pemba katika mkutano wa utoaji wa uelewa wa
kodi ya majengo huko baraza la Wawakilishi Wete mkoa wa Kaskazini Pemba amesema
ulipaji wa kodi ni moja ya chanzo kitakachoipatia Nchi kupiga hatua
kimaendeleo.
Alisema
masheha wana nafasi kubwa katika jamii, hivyo ni jukumu lenu kuwaelimisha
wananchi ili kuhakikisha wanatekeleza juku lao la ulipaji wa kodi.
‘’Ndugu
zangu masheha ni wajibu wenu kutoa elimu kwa jamii ili kuona wanatekeleza
wajibu wa Serikali wa ulipaji wa Kodi,’’alisema.
Aidha kwa upande mwengine alifahamisha kuwa miongoni mwa majengo yatakayolipiwa kodi ni
majumba ya Ghorofa pamoja na majengo
yanayotumika kwa ajili ya biashara, na sio majengo mengine ya kawaida.
‘’Kodi ya
majengo haiwahusu Wananchi bali itawahusu wenye nyumba za ghorofa tu, ikiwa
yanatumika kwa biashara na hata kwa ajli ya makaazi,’’ alifahamisha.
Alisema
majengo ya ghorofa yanayotumika kwa ajili ya makazi yatalipiwa Shilingi
10,000/= kwa mwaka kwa kila jengo moja,,.
Majengo ya
biashara yenye ghorofa yatalipiwa Shiling 50,000/=, ambapo majengo mengine
yasio ya biashara yatalipa 50,000/=.
Na majengo
ya Hoteli za ghorofa zitalipa kulingana na hadhi ya majengo hayo.
Akifungua
mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib amemtaka
Kamishna wa [ZRA] Zanzibar kuendelea kutoa elimu kwa watu mbali mbali kuhusu
sualala kodi ya majengo ili kuona
Wananchi wamepata uelewa wa kutosha juu ya suala hilo.
Comments
Post a Comment