RUSHWA MUHALI BADO NI TATIZO KWA JAMII
NA FATMA
HAMAD PEMBA.
Imebanika
kuwa rushwa muhali bado
ni kilio kikubwa
kinachoendelea kuikumba jamii
hali ambayo inapelekea kesi
nyingi za udhalilishaji
kufutwa Mahakamani kutokana
na kukosa ushahidi.
Wakizungumza katika mkutano wa
robo mwaka wa kujadili juu
ya utekelezaji wa
majukumu yao wana mtandao wa
kupinga udhalilishaji kutoka wilaya ya
Mkoani huko ukumbi wa Chama cha
Wandishi wa habari Wanawake Tanzania
[Tamwa] iliyopo chake chake Pemba.
Wamesema licha
ya juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali pamoja na
wanaharakati mbali mbali ya
kuwafahamisha jamii kufahamu madhara ya
udhalilishaji lakini bado juhudi hizo zinagonga mwamba.
Wamesema wamebaini kuwa wengi wafanyaji wa matukio hayo huwa ni ndugu wa familia moja, hivyo huzimalizia mitaani hawaendi
kutoa ushahidi kwa kuhofia ugomvi katika
familia zao.
‘’Sasa hivi
kunapotokezea udhalilishaji huamua kupigishana faini wenye kwa wenyewe
majumbani hawendi katika vyombo vya sheria kwa kuogopa mtuhumiwa asije akafungwa’’
walisema wadau.
Walisema
licha ya kuwa shahidi ambae amefanyiwa
udhalilishaji atatoa ushahidi wake vizuri
katika hatua za awali mwisho wa
siku hupewa sumu ili kukanusha ushahidi alioutoa ilimradi tu uonekane kuwa ni wa uongo.
Kwa upande wake Rashidi Mshamata kutoka wilaya ya wete amsema ili kuondosha hilo nivyema Serikali kuweka nyumba salama za kuwekwa mashahidi ambao pia ni wathirika wa matukio hayao.
‘’Shahidi
akirudi kwenye jamii yake anapikwa anaiva hatoi ushahidi wa kweli, na laiti zingelikuepo
hizo nyumba salama tungefanikiwa’’ alisema Rashid.
Nae mratibu
chama cha wandishi wa habari Wanawake [TAMWA] Ofisi ya Pemba Fathiya Mussa Said
amewashauri wanamtandao hao pamoja na
wandishi wa habari wasivunjike moyo waendelee kuielimisha jamii ili kuondoka na
udhalilishaji hapa Nchini.
Jumla ya
kesi 10 za udhalilishaji wa kijinsia zimeibuliwa na wanamtandao hao katika
wilaya ya Mkoani kwa kipindi cha January hadi Mei mwaka huu.
Comments
Post a Comment