WALIMU WA MADRASA WAENDELEZA VIPAJI VYA QUR AN

Walimu wa madrasa za Qurani  pamoja  na wazazi  wametakiwa kushirikiana kwa   pamoja  kuwasimamia  watoto  wao  kuhakikisha  wanaendeleza   suala la uhifadhi wa Qurani   ili kupatikana vipaji  vyenye ubora.

Hayo yamesemwa na Mmoja wa wazazi  wa wanafunzi  wa madarasa za kurana  Ali Hamad Bakari  katika hafla ya mashindano ya tahfidh lkuran yaliofanyika Viwanja vya mpira Pwepweu viliopo  Tumbe wilaya ya Micheweni Mkoa waKaskazini Pemba  amesema uhifadhi wa kurani ni suala muhimu kwani hupelekea  kuwepo  na kizazi  chenye  madili.

‘’Mashirikiano ya pamoja ndio njia pekee inayopelekea wanafunzi kuendeleza masomo yao na kuibua vipaji’’ alieleza mzazi.

Akitoa nasaha zake mara  bada ya kumalizika kwa mashindano hayo Msaidizi  wa Katibu  mtendaji Ofisi ya Mufti mkuu upande wa Pemba Said Ahmad amewawataka walimu wa madrasa   kuliendeleza  suala  la uhifadhi  wa guranai  ili kuviendeleza viapaji  hivyo ili kuweza kukipatia sifa nzuri Kisiwa cha Pemba.

Mashindano hayo yamefadhiliwa  Jumuia ya Falmunir Khalid Fondation yenye makazi yake Darsalam.


Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.