ZAFELA YAWA MSAADA KWA WATOTO WA KIKE WALIOACHA SHULE

 

NA FATMA HAMAD,

Mkurugenzi wa Jumuia ya  Wanasheria  wanawake Zanzibar  Zafela  Jamila Mahmoud,  amezitaka asasi za kiraia kushirikiana kwa Pamoja na kuwajengea uwezo Watoto wa kike,  walioacha Skuli  ili  waweze  kurudi shuleni na kuendelea na masomo yao.

Mkurugenzi huyo aliyasema hayo katika mkutano wa kuutambulisha mradi wa Malala, utakaoendeshwa na Zafela visiwani Zanzibar  kwa muda wa mwaka mmoja, kikao hicho kilichowajumuisha asasi mbali mbali za kirai kisiwani Pemba.

Alisema katika utafiti wao walioufanya  waligundua kuwa ,kuna  wimbi kubwa la watoto wa kike  wamekuwa wakikatisha  masomo yao kutokana na sababu mbali mbali, ikiwemo kuolewa, kupata mimba za utotoni Pamoja na kufanyishwa  kazi za nyumbani.

Alisema wamekuwa wakipokea kesi nyingi za Watoto wa kike, kuda haki zao, aidha waliolewa au waliojihusisha na mahusiano, ambao ukiwangalia umri wao  unapaswa   wawe wako shuleni na wanaendelea na masomo yao.

‘’Tumeamua kuleta mradi huu wa Malala  kwa ajili ya kumuezesha na kumsaidia  mtoto wa kike ili aweze kurudi shule na kumaliza  masomo yake  angalau hadi darasa la kumi na mbili,’’alisema mkurugenzi.

Alifahamisha kuwa  mrahidi  huo umelenga kuwafikia jumla ya Watoto  3000 kwa  Unguja na Pemba, hiyo amezitaka asasi za kiraia kuweka mashirikiano makubwa  na jumuia ya Zafela ili kuona mradi huo umefikia malengo.

Aidha kwa upande mwengine  mkurugenzi aliwataka wanajamii kukaa karibu na Watoto wao na kuwasikiliza matatizo yao, ili wawe na uthubutu wa kueleza changamoto zinazowatokezea katika harakati zao za kimasomo.

‘’Inawezekana mtoto anaacha Shule kutokana na vikwazo tu vinavyo mkwaza aidha njiani au shuleni, hiyo tujenge urafiki na Watoto wetu ili tuwanusuru na kadhia kama hizo,’’ alifahamisha mkurugenzi.

Mapema msimamizi wa mradi huo Hairun Abass Rajab kutoka  chama cha wanansheria  wanawake Zanzibar [Zafela] Alieleza kuwa hadi sasa bado zipo familia ambazo hazimpi fursa mtoto wa kike kupata haki yake ya elimu kuanzia Msingi hadi Vyuo vikuu.

 

 Alifahamisha kuwa lengo la mradi huo nikuwasaidia Watoto walioacha Shule, na waliokatika mazingira magumu, ili kuhakikisha wanapata elimu na kufikia ndoto zao.

Akichangia katika mkutano huo mwanaharakati wa kulinda na kutetea  haki za wanawake na Watoto kutoka wilaya ya Mkoani  Sada Moh’d Othman alisema ni vyema kuweko na mkakati Madhubuti ya kuwaekea usimamizi wa hali ya juu   wanafunzi hao wakati watakapo rudi shuleni ili kunusuru vitendo viovu na waendelee na masomo yao.

‘’Kuna Watoto waliokaa nje kwa muda mrefu, na tayari walisha athirika na ulevi, ulawiti, ubakaji, hivyo ni vyema tuwe makini nao, wakati tunapowarejesha shuleni, ili wasije wakambukiza na wengine,’’alifahamisha mwanaharakati.

Nao washiriki Ali moh’d Ali na Salim Said walisema ili kumaliza  vitendo viovu  katika jamii, ni lazima kila mmoja kwa nafasi yake  kuchukua jitihada za makusudi, jambo ambalo litasaidia kupata kizazi  chenye madili mema.



Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.