WANDISHI WAPEWA NENO
NA FATMA HAMAD PEMBA.
Wandishi wa
habari wametakiwa kutoa elimu kwa jamii ili kufahamu umuhimu wa afya ya uzazi.
Wito huo umetolewa na Afisa mdhamini wizara ya afya wakati akifunga
Mafunzo ya Siku tatu yanayo husu afya ya Uzazi kwa wandishi wa habari huko katika ukumbi wa Chama cha Wandishi wa habari Wanawake
Tanzania [TAMWA] Chake chake Pemba.
Alisema imeonekana bado jamii haina uwelewa wa kutosha kuhusu afya ya uzazi,jambo ambalo linachangia kukosa afya bora ya mama na mtoto.
‘’Ndugu zangu nyinyi wandishi wa habari ndio kioo kwa
jamii, hivyo tunaomba mtusaidie kuielimisha jamii jambo ambalo litaepusha Vifo
vitokanavyo vya uzazi,’’ alisema mdhamin bilali.
Aidha aliiasa
jamii kuacha tabia ya kuwaozesha waume mabinti
zao ambao hawajafikia umri wa miaka 18, kwani kutawaepusha na matatizo mbali
mbali yatokanayo na uzazi.
‘’Siku hizi kuna matatizo mengi jamani yatokanayo na
uzazi, hivyo wazazi tuacheni tamaa ili tuwakinge watoto wetu,’’ alifahamisha
mdhamin.
Mapema Afisa Miradi na Tathmini kutoka Chama Cha
Waandishi wa Habari Wanawake Ofisi ya Pemba, Mohammed Khatib Mohamed amesema
mafunzo hayo yameletwa ili kuwajengea uwezo waandishi wa Habari ili kuielimisha jamii
kuhusu masuala ya afya ya uzazi.
Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo
mkufunzi kutoka kitengo Afya Dr Rahila Salim Omar amewashauri wananchi kutumia uzazi wa mpango katika
kuimarisha afya zao.
Nae Mkufunzi wa mafunzo hayo Ali Mbarouk Omar aliwataka wanajamii kufika hospitali, kupima afya zao na kupatiwa
matibabu pindi watakapo gundulika na matatizo.
Comments
Post a Comment