UFAHAMU UZAZI WA MPANGO
Wananchi kisiwani Pemba wameshauriwa kutumia njia salama ya uzazi wa mpango hali ambayo itasaidia kuimarisha afya ya mama na mtoto.
Ushauri huo umetolewa na mtaalamu wa masuala ya Afya ya uzazi Rahila Salim Omar kwa wandishi wa habari kisiwani Pemba alisema zipo njia kadhaa za kupanga uzazi ambazo zote ni salama.
Alisema miongoni mwa njia hizo ni zile za kisayansi pamoja na za kisasa ambapo hazina madhara yoyote.
Alisema miongoni mwa njia hizo ni kama vile kitanzi kwa mama ambaye hajajifungua sana, sindano,vipandikizi,vidonge ambazo zote ni salama na hutolewa kulingana na afya ya mama.
''Sio kweli kwamba ukipanga uzazi unapata matatizo tusidanganyane, kitalamu hakuna hilo njia zote zipo salama, alifahamisha docta Rahila''
''Kisheria mtoto anatakiwa anyonye miaka miwili, ndipo mama abebe ujauzito,'' ili kuimarisha afya ya mama na mtoto, "alifahamisha sheikh Nassor.
Aidha alifahamisha kuwa njia za kufunga uzazi zipo kwa wanawake na wanaume sio kwa wanawake tu, hivyo ni vyema wanaume nawao kuzitumia njia hizo.
ReplyForward |
Comments
Post a Comment