DC MICHEWENI APIGA VITA UNYANYAPAA DHIDI YA WATOTO WENYE ULEMAVU
NA FATMA
HAMAD -- PEMBA.
Wazazi na
walezi wenye watoto
wenye ulemavu wametakiwa
kuwapeleka Skuli pamoja na
madrasa ili nawao waweze kujipatia haki yao ya elimu kama watoto wengine.
Kauli hiyo
imetolewa na mkuu wa wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya wakati akizungumza
na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya
simu alisema bado wapo wazazi wanatabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu na badalake
kuwakosesha haki zao.
‘’Niwaombe
wazazi waache tabia ya kuwafungia ndani watoto wenye ulemavu kwani nawao ni binadamu kama wengine wanahitaji kupata
haki zote stahiki, ’’alisema mkuu wa Wilaya.
Alieleza
wapo wazazi katika jamii wanapozaa watoto
wenye ulemavu wamekuwa wakiwanyanyapaa
na kuhisi kama ni mkosi ndani ya familia yao, jambo ambalo haileti picha nzuri
kwa mwenyewe mwenye ulemavu na hata kwa Mwenyezi Mungu.
Alifahamisha
watoto wenye ulemavu waliowengi wanapenda kusoma na mara nyingi Mungu huwajaalia
kipaji, hivyo ni budi wapatiwe fursa
mbali mbali ili waweze kutimiza malengo yao waliojiwekea.
‘’Tusiwatenge
tuwapeni fursa watoto wetu wenye ulemau
ili nawao wawemo katika Sekta mbali mbali jamani, tutakwenda kuulizwa kesho
mbele ya Allah(S,W)’’ alieleza mkuu wa wilaya.
Mapema sheha
wa shehia ya Shumba ya vyamboni Time Said Omar alisema wanachukuwa jitihada
mbali mbali ya kuwaelimisha jamii kuhakikisha wanawalinda na kuwapatia matunzo
watoto wenye ulemavu.
Aidha
aliwataka wananchi kutoa taarifa wakati watakamuona mtu mwenye ulemavu yoyote
ananyanyapaliwa ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
Nae mama
mzazi wa Abdala Hussein Rashid mwenye
ulemavu wa viungo Bi Time Kombo
Juma mkaazi wa Kwale gongo alisema licha ya ulemavu wake alionao mtoto wake lakini hakumbagua alimpeleka madrasa, skuli na
sasa ni mwanafunzi wa darasa la kumi katika skuli ya Sekondari kinyasini wilaya
ya wete kaskazini Pemba.
Hivyo
aliwataka wazazi wenzake wenye watoto
wenye ulemau wasikate tamaa waige mfano wake, wawasomeshe na wawapatie fursa
mbali mbali ambazo zitaleta maendeleo kwao kwani nawao wanauwezo wa kufanya
kazi.
Katiba ya
Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 12[1] kinasema ‘’Watu wote ni sawa mbele ya
sheria, na wanayohaki bila ya ubaqguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa
mbele ya sheria.
Comments
Post a Comment