WANAFUNZI MASKULINI WAPEWA NENO.


NA FATMA HAMAD PEMBA.

Wanafunzi   wametakiwa  kuwa mstari wa mbele  kutoa  tarifa  kwa  walimu au wazazi wao wakati watakapoona  viashiria  vya udhalilishaji katika maeneo yao.

Wito huo umetolewa na Msaidizi wa Sheria kutoka Jumuiya ya wasaidizi wa Sheria Wilaya ya Micheweni Said Salum Khamis  alipokuwa akitoa elimu juu ya mapambano dhidi ya ukatili na udhalilishaji  watoto huko skuli ya  Sizini  ikiwa ni shamra shamra ya madhimisho ya siku   ya mtoto wa afrika.

Alisema  vitendo vya udhalilisha vinafanyika katika mazingira ya jamii hivyo wakati umefika kwa wanafunzi kuondosha  muhali bali watoe tarifa  pale wanapoona vitendo vya udhalilishaji ili viweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

‘’Sasaivi udhalilishaji unafanyika  kila  pahala hivyo msiogope toeni tarifa msiogope’’ alisema Said Salum.



Mapema Sanani Said Salum kutoka jumuia hiyo Wilaya ya Micheweni amewahimiza wanafunzi hao  kushughulikia masomo zaidi  na kujiepusha na vishawishi vinavyoweza kuwasababisha kutumbukia kwenye dimbwi la  vitendo viovu vikiwemo uhasharati, ulevi na ujambazi.

 Nae kwa upande wake afisa jinsia  na watoto wilaya ya micheweni Bizume Haji Zume amesema lengo la kutoa elimu hiyo  ni kufikisha ujumbe kwa wanafunzi juu ya kuisoma katiba ya  Nchi ili waweze kuzitambua na kuzifahamu haki zao za msingi  wanazostahiki kuzipata katika maisha yao.

Utoaji wa elimu hiyo dhidi ya  ya ukatili wa watoto ikiwa ni shamra shamra ya madhimisho ya siku ya mtoto wa afrika ni ushirikiano wa Jumuia za wasaidizi wa sheria, Chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania [TAMWA] na Kituo cha huduma za sheria Zanzibar.

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.