WANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUZISOMA SHERIA

 




NA FATMA HAMAD PEMBA.

Wandishi  wa  habari   wametakiwa  kuzisoma na kuzifahamu sheria  mbali mbali  ili waweze kuandika habari  zenye  ukweli ambazo zitaleta  tija kwa jamii.

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya  Mkoani Khatibu Juma Mjaja wakati akizungumza na wandishi wa habari katika mafunzo ya kujadili sheria ya habari huko gombani Chake chake Pemba.

Amesema wandishi wa habari ni wadau wakubwa ambao mnaweza kuiletea nchi mabadiliko hivyo ni muhimu  kuzifahamu kanuni na sheria  ambazo zitawaongoza kuandika habari zenu kwa kuzingatia madili.

‘’Nyinyi wandishi wa habari ni wadau muhimu katika Nchi  hivyo ni lazima muzisome sheria ili muweze kuwa wadilifu katika kazi zenu’’ amesema Mkuu wa wilaya.

Katibu mtendaji kutoka baraza la habari Tanzania [MCT]  Kajubi Mukajanga  amesema  kutokuzifahamu sheria sio kinga ya kutokuadhibiwa wakati unapoivunja,  hivyo ni lazima musome sheria ili muepuke  kuandika habari zenye  kusababisha migogoro.

‘’Msipo zifahamu sheria  mtandika habari ambazo zitaleta migongano’’ amesema  katibu mtendaji.

Kwa upande wake  mwenyekiti wa baraza la habari Tanzania [MCT] upande wa Zanzibar Shifaa Said Hassan amesema endapo wandishi wa habari watazifahamu sheria  pamoja na vifungu vya Katiba kutawawezesha  kuibua   habari  zenye kuaminika na zenye kuifanya  nchi kupiga hatua kimaendeleo.

Kwa upande wake Ofisa mdahamini wizara ya habari vijana na Michezo  Mfamau Lali mfamau amesema  wandishi wa habari wasiandike habari kwa mazoea, hivyo basi wakati umefika kubadilika  ili waendane na soko la Dunia.


Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.