WANAOHARIBU USHAHIDI WAONYWA
Serikali ya
mkoa wa Kusini pemba imesema
haitomvumilia mtendaji
yoyote atakaebainika anashiriki kuharibu ushahidi wa kesi ya
udhalilishaji kwa makusudi ili kesi hiyo
isiendelee mahakamani.
Kauli hiyo
imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Masoud katika madhimisho
ya siku ya Mtoto wa Afrika huko Gombani
Chake chake Pemba.
Amesema wapo baadhi ya watendaji wakiwemo Madaktari hawataki kwenda mahakamani
kutoa ushahidi hivyo hatutokubali
tutawachukulia hatua kali za kisheria
watakao kataa kutoa ushahidi.
‘’Wapo
madaktari ambao mnawafanyia
uchunguzi wanaodhalilishwa hamtaki kwenda kutoa ushahidi, lakini
nimeshaliagiza jeshi la Polisi liwaweke ndani madaktari watakao kataa’’alisema
mkuu wa Mko
Amesema vitendo vya udhalilishaji vimeshakua tishio kwa jamii hivyo kama watu watakataa kutoa ushahidi hakuna kesi itakaopata hatia na badalayake tutaendelea kuibebesha mzigo wa lawama mahakama kwamba haitendi haki.
Mapema Ofisa mdhamini wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali Pemba Muhamed Nassor Salim amesema bado Jamii yenyewe haijakua tayari kupiga vita vitendo vya udhalilishaji.
‘’Sheria
zetu ziko makini, watendaji wetu wako makini lakini jamii bado haijakua na
sauti ya pamoja ya kusema sasa udhalilishaji basi’’ alisema Afisa mdhamini Elimu.
Akisoma
Jumla ya matukio 130 ya udhalilishaji yameripotiwa kuanzia Jane mwaka hadi March mwaka huu katika mkoa wa Kusini Pemba.
Comments
Post a Comment