WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUWANZISHA MIRADI AMBAYO ITAWALETEA MAENDELEO

 
 NASALIM HAMAD PEMBA.

Kaimu mkurugenzi wa Jumuiya ya Wasaidizi wa Sheria wilaya ya Micheweni [Midipao] Saleh Hamad Juma amewataka wajasiriamali kuanzisha miradi kama vile utengenezaji wa Sabuni,Ukulima wa mboga ili waweze kujipatia faida itakao saidia kuendesha vikundi vyao.

Ushauri huo ameutoa wakati akizungumza na wanakikundi cha kueka na kukopa cha Hatusemani kilichopo  Tumbe kaliwa wilaya ya Micheweni mkoa wa Kakazini Pemba katika kikao maalumu kilichoandaliwa na jumuiya hiyo cha kuishajiisha jamii kujiunga na vikundi vya ujasiriamali.

Alisema endapo watazalisha Sabini, au kujingiza kwenye kilimo cha mboga mboga watajipatia kipato na kukuza vikundi vyao kupiga hatua kimaendeleo.

‘’Niwaombe mama zangu musishie tu kuja mukiweka pesa na kuondoka, bali anzisheni miradi ili muweze kuviendeleza vikundi vyenu pamoja na kujipatia kipato ambacho kitainua maisha yenu, alisema.

 Aliendelea kusema endapo watazalisha bidhaa zenye ubora ambazo zitaendana na soko la dunia wanaweza kupata ufadhili kutoka Nchi mbali mbali Duniani.

 Kwa upande wake Msaidizi wa Sheria shehia ya Tumbe Mashariki Fatma Hamad Faki aliwataka wanakikundi hao kuichangamkia Fursa ya Mikopo  iliyotolewa na Serikali ya Mapinduzi ili kuona wananufaika nayo.

‘ Serikali ya Mapinduzi kwa kuwajali wananchi wake imeweka fursa ya kuwapatia mikopo Wananchi wake ili waweze kujiendeleza kiuchumi, hivyo ni haki yetu na  sisi tukajipatipatia mikopo hiyo, alieleza.

Alifahamisha kuwa mkopo huyo ni haki ya kila mtu alimradi tu uwe umetimiza vigezo na masharti iliyowekwa kisheria.

 Nae Mwenyekiti wa kikundi hicho Bi Suria alishukuru Jumuiya ya wasaidizi wa sheria ya Micheweni kwa kuwapatia elimu hiyo, huku akiahidi kuifanyia kazi na kuona wanatimiza ndo zao za kuondokana na umasikini.


 

    

 

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.