WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUJIUNGA NA MAJUKWAA YA WANAWAKE

 

NA, FATMA HAMAD-PEMBA


Mkurugenzi  Idara ya Maendeleo  ya Jamii Jinsia wazee na Watoto Zanzibar Siti Abasi Ali amewataka Viongozi wa Majukwaa ya Wajasiriamli Wanawake Kisiwani Pemba kuhakikisha wanavishajihisha Vikundi Vya Ujasiriamali kujiunga na Majukwaa hayo  ili viweze kuwezeshwa kwa  kupatiwa mikopo ya kujiendeleza kiuchumi.

Mkurugenzi  huyo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wenyeviti wa Majukwaa wa wilaya Nne za Pemba katika hafla ya ufunguzi wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo wajasiria mali hao.

Alisema Vikundi vitakapo jiunga na majukwaa hayo itakuwa rahisi kupatiwa mikopo ya kujiendeleza katika harakati zao .

Alisema Serikali imeaanzisha majukwaa ya Wajasiriamali wanawake kwa ajili ya kuwaunganisha Pamoja na kuwa na sauti moja ili waweze kujadili shida walizonazo .

Alisema hatua hiyo itakuwa rahisi kuweza kuwafikia kwa wepesi katika kuwasidia kwa kuwapatia mitaji ya kujiendeleza kiuchumi, ili  waondokane na utegemezi na unyanyasi wanaoupata katika jamii au kwenye ndoa zao.

Aidha alisema Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo juu ya  namna bora  ya kuendendesha  biashara zao   baada ya kupatiwa mikopo  wajasiriamali hao.

Alieleza kuwa baadhi ya  wajasiriamali hawana elimu ya kutosha katika kuendeleza biashara zao na ndio maana wakatoa mafunzo hayo waweze kujiendesha baada ya kupatiwa ruzuku.

Hata hivyo aliwatahadharisha akina mama hao wakati watakapo patiwa mikopo wahakikishe wanazitumia kwa misingi iliyokusudiwa na sio kuwachia waume zao kuongeza wake.



Kwa upande wao washiriki wamafunzo hayo walisema watayatumia vyema  huku  wakiahidi kuongeza Vikundi  kwenye jukwaa hilo ili viweze kunufaika  na ruzuku inayoweza kutokea.

Raya Mohamed Khamis ni miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo alisema mafunzo hayo yamewafumbua macho katika namna ya kujiendeleza kiuchumi na kuahidi kuyatumia ipasavyo.

Mafunzo hayo yamewashirikisha wenyeViti wa Majukwaa ya Wajasiriamali wanawake kutoka Wilaya Nne za Pemba.



Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO