TAMWA YAIBUA KASORO SHERIA ZA KUPAMBANA NA UDHALILISHAJI
13/2/2023.
NA FATMA HAMAD PEMBA
KATIKA kupiga
vita suala la udhalilishaji wa
kijinsia, Serikali imeweka mikakati
mbali mbali, ikiwemo kufanya marekebisho
ya sheria, ambazo zinahusu
masuala ya udhalilishaji
wa kijinsia, ili kuona
jamii inaondokana nalo.
Lakini licha
ya marekebisho hayo
bado vipo vifungu
kadhaa vya sheria, ambavyo
vinaonekana bado vina mapungufu na vinaleta ukakasi juu ya uendeshwaji na utolewaji wa
hukumu kwa kesi za udhalilishaliji katika vyombo vya sheria.
WANAJAMII.
Kombo Ali
Hamad mwanajamii kutoka wilaya ya Wete, amesema mtu yoyote atakae mnajisi mtu
mwenye ulemavu asipewa dhamana kifuatwe kifungu cha 151 [1] cha sheria 7 ya
2018 sheria ya Mwenendo wa makossa ya Jina, kwani wenye ulemavu na wao ni bidamu na linathirika zaid kundi hilo .
‘’ Mimi kwa
maoni yangu nashauri icho kifungu
kinachozungumzia atakae mnajisi mgonjwa wa akili apewe dhamana, kifutwe
kwani hakiwatendei haki watu wenye ulemavu,’’ alisema Kombo Ali Hamad.
Watu wate
wafuate sheria bila shuruti, hivyo yoyote atakaemdhalilisha mtu mwenye mlemavu
wa akili, achukuliwe hatua na kupewa adhabu kwa mujibu wa sheria invyoelekeza.
Akashauri
kuwa, asiachiliwe kwa sababu tu isionekanwe kama aliyemfanyia hana akili,
mtazidi kuwapa nafasi ya kuwadhalisha.
Hidaya Mjaka
Ali mwenye ulemavu wa viungo mkaazi wa shehia ya Vitongoji, amesema kwa sasa
kifungu hicho kinachosema atakae mnajisi mlemavu wa akili apewe dhamana,
hakifai.
Anasema, kwani
anapokuwa nje anaweza akafanya chochot
ili aweze kuharibu ushahidi, hivyo ni vyema nae asipewa dhamana.
‘’Mimi
kifungu hicho nakiona hakiko sawa, naomba kifutwe kabisa hakifai, kwani licha ya kuwa ni mlemavu wa akili,
lakini ni vyema kw amtuhumiwa awekwe ndani, mpaka utakapomalizika kwa ushahidi na
ikithibitka hajafanya atatolewa,’’anasema.
Mara nyingi
kesi za watu wenye ulemavu zinapotokezea
huishia njiani na hizo sheria zikiwa na mapungufu watu wanazidi kupata chaka la
kujifichia wakazidi kuwadhalilisha watu wenye ulemavu.
MZAZI WA MTOTO MWENYE ULEMAU
ALIEDHALILISHWA
Mimi
mwakajana mtoto wangu mwenye ulemau wa akili na matamshi alibakwa na kupewa ujauzito, nikaenda kwa
sheha na kesi akaifikisha kituo cha Polisi
Konde.
Mama huyu
mkaazi wa Tumbe hakuona tabu alisema atasimama mpaka haki ya mwanangu
ipatikane nikaenda polisi siku ya kwanza nikambiwa niende siku nyengine.
Ilipofika
siku niliopangiwa simu alikwenda na
mwanangu akaitwa akatoa ushahidi wote, ila kwa kweli kwa mazingira niliyoyaona alikata tamaa na kujua kuwa kesi ya
mtoto wake haifiki popote.
‘’Mwisho wa siku kesi ilifutwa katika kituo cha Polisi Konde
mtuhumiwa yuko anaendelea na shughuli zake mtaani bila ya wasi wasi wala hofu,’’
alieleza mama huyo.
ALIEFANIKIWA KESI YAKE BAADA YA MDOGO
WAKE KUDHALILISHWA
Mimi mdogo
wangu mwenye ulemavu wa akili, mara baada ya kunajisiwa na Nuhu Kombo mkaazi
wa Kijichame, niliipeleka kesi kituo cha polisi Micheweni, akaambiwa asubiri
wanaendelea na upelelezi.
Anasema baada
ya kumaliliza upelelezi wao, aliitwa kituoni na muathirika na kuanza kuchukuliwa
maelezo.
‘’Sikukata
tamaa niliendelea kuifuatilia kesi hiyo na kisha ilifikishwa mahakamani na sasa
mtuhumiwa yuko Chuo cha Mafunzo akitukimia miaka saba (7).
WANAHARAKATI
Wanaharakati
wa kupambana na masuala ya udhalilishaji, wamekuwa wakizipigia kelele sheria
ambazo zinaonekana na mapungufu yanayopelekea uzoroteshwaji na ukosekanaji wa
haki za wathirika wa vitendo vya udhalilishaji.
Fathiya
Mussa Said kutoka TAMWA- Pemba amesema suala la kupewa dhamana kwa mtu atakae
mnajisi mwenye ulemavu wa akili, ni tatizo na ipo haja
ya kutokupewa dhamana.
‘’Tunaomba
kifuatwe kifungu cha 151 [1] cha sheria 7/ 2018 na kifungu cha 116 cha sheria 6
/2018 kirekebishwe isiwe sababu ya
kupewa dhamana kwa sababu tu, amemfanyiwa
mtu mwenye ulemavu wa akili, tukifanya
hivyo tutaendelelea kuwadhalilisha na
kuwakosesha haki zao.
JUMUIA YA WATU WENYE ULEMAVU WA AKILI
[ZAPDD]
Khalfan
Amour Mohamed ni Mratib wa Jumuia kwa ajili ya ya watu wenye ulemavu Zanzibar
‘ZAPDD’ kisiwani Pemba, anasema kuwa ni
vyema sheria ingetoa tafsiri halisi ya neono
la kunajisi, ili kujua nikupi huko, vyenginevyo kiingizwe kwenye kifungu cha 151 cha sheria
7/2018 sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
‘’Tunataka tufahamu kifungu hicho cha 116 cha sheria namba 6/ 2018 sheria
ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, jee kinawahusu watu wenye ulemavu wa kili tu,
kwani hawa wao si binadamu hawana haki kwenye taifa hili,’’alihoji.
Sisi wadau
wa watu wenye ulemavu tunataka kifungu cha 116 kifutwe kabisa, kwani kinaleta
utofauti wa watu wenye ulemavu wa akili na wasio na ulemavu, tunataka kosa hilo
liingizwe kwenye kifungu cha 151 kinachozungumzia dhamana.
Hakimu wa mahakama maalumu ya kupamba na makosa
ya udhalilishaji mkoa wa Kusini Pemba, Muumin Ali Juma amesema kesi za watu
wenye ulemavu bado ni changamoto kubwa,
na mara nyingi hufutwa kutokana na kukosa ushahidi.
‘’Ukosefu wa
wakalimani ni kikwazo kikubwa, kinachopelekea kesi nyingi za watu wenye ulemavu
kushindwa kupatatiwa,’’ alisema hakimu Muumin.
Kifungu cha (151) [1] cha sheria namba 7 ya
mwaka 2018 cha sheria
ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai,
sheria ya Zanziba
kimeorodhesha makosa ambayo hayana
dhamana, ikiwa ni kubaka,
kuingilia kinyume na maumbile, kumuingilia maharimu, kubaka kwa kikundi,
kumnajisi mtoto wa kiume.
Lakini kosa
la kumnajisI mtu mwenye ulemavu wa akili lililopo kifungu cha 116 cha sheria
namba 6 ya mwaka 2018, kosa hili lina dhamana,
sheria hiyo
imeonekana na kasoro hivyo wadau pamoja
na anaharakati mbali mbali
wa kutetea masuala ya
udhalilishaji wakitaka kifutwe.
Tunataka
kuwepo na sheria moja tu ambayo itajumuisha makosa yote ya udhalilishaji
badala ya kuepo na sheria tofauti tofauti kwenye kosa moja.
KATIBA YA ZANZIBAR.
Katiba ya
Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 12 [1] kinasema watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki bila
ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawambele ya sheria, ikiwa katiba
inasema hivyo, lakini bado watu wenye ulemavu wanaona wanabaguliwa juu ya kifungu cha 116 cha
sheria 6 / 2018 mtu akimnajisi mwenye ulemavu wa akili anapewa dhamana, lakini kifungu
cha (151) [1] cha sheria namba 7 ya mwaka 2018
cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, sheria
ya Zanziba kinasema kuwa akinajisiwa
mwenye akili zake timamu hapewi dhamana.
Comments
Post a Comment