UKOSEFU WA WALIMU MJUMUISHI UNAVYOATHIRI NDOTO ZA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU PEMBA

 

                           NA FATMA HAMAD, PEMBA

‘’Namshukuru nimefaulu mtihani wangu wa darasa  la kumi  na leo nipo  darasani na jumuika na wenzangu, kuchota elimu hapa skuli ya sekondari Kinyasini,’’anasema mwanafunzi.

Hayo ni maneno ya mwanafunzi Hussein Abdalla Rashid  mwenye ulemavu mchanganyiko mkaazi wa Kwale gongo wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba.

Abdalla ni mwanafunzi ambae anaisaka elimu katika mazingira magumu, kwani anakotoka kijiji cha mbali na kwenye mabonde na milima.

‘’Ninatoka kjiji cha mbali ambapo ni kilo mita 10, kutoka nyumbani kwetu hadi skuli, ila sijali  kwani ndoto yangu ni kuwa fundi wa umeme,’’ alisema Abdala.

CHANGA MOTO ZA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU

Abdalla Husein Rashid amesema kuwa anatamani siku moja  awe  fundi  mkubwa  wa  umeme,  lakini bado  wanakilio  kwenye Skuli zao  hakuna  walimu  wa kufundisha  wanafunzi wenye ulemavu.

Amesema kitendo cha  wanafunzi wenye ulemavu kuchanganywa  darasa  moja na wasio na ulemavu  huku wakiwa hawana  mwalimu wa kuwasaidia ni kikwazo  kwa wanafunzi  wenye ulemavu.

‘’Mfumo wa elimu mjumuishi wa kutuchanganya darasa moja sisi wenye ulemavu na wasio na ulemavu bado hauja tutendea haki kwani hatuna walimu wa kutufundisha,’’ alisema.

Alisema kwa kweli hakua   na tamaa ya kufalu darasa la kumi  kwa sababu  toka anze darasa la kwanza, hadi kufikia hapo hajapatapo  mwalimu  hata  siku  moja  wa kumsaidia.

‘’Mimi nangalia tu ubaoni kinachoandikwa  ndio naweka kichwani  si fahamu chochote  mwalimu  anachofundisha  ila tu mungu na rehema zake amenijalia nimefaulu’’.

 Hivyo  wamemuomba rais wao mpendwa kukiona  na kukifanyia kazi kilio  chao na kuwawekea mazingira rafiki ili nawao watimize ndoto zao.


Mohamed Karume mwanafunzi  wa  darasa la saba  skuli  

ya sekondari  Utaani  Wete  Pemba  mwenye  ulemavu  wa  viungo  ameeleza  kuwa  anandoto  ya  kuwa  Mhandisi majengo.

  Amesema  ili aweze  kutimiza  ndoto  yake  hiyo  ni  vyema serikali  ikawajengea skuli yao malumu na kuwawekea miundombinu  ya  kutosha,  kama  vile walimu  wa  lugha  za  amala, vitabu vya kufundishia pamoja na kuwapatia misaada ya viti mwendo.

‘’Licha ya ulemavu wangu  lakini  nasoma kwa  bidi,  kwani nina hamu ya kuwa ‘injinia’ mkuu wa majengo,  namuomba rais wetu  atuangalie kwa  jicho la huruma na sisi tunayo haki  na tuna uwezo mkubwa wa kuleta maendeleo,’’ alielezea

WALIMU WA SKULI

Mwalimu  mkuu skuli ya Kinyasini iliyopo Wete Pemba Asha Mbarouk Rashid, amekiri kuwepo kwa kadhia hiyo ya ukosefu wa mwalimu anaejua lugha za alama kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu.

Hivyo aliomba Wizara ya elimu na mafunzo ya amali, kuwapa kipaumbele wallimu waliosomea elimu mjumuishi katika ajira jambo ambalo litasaidia kuondosha tatizo hilo maskulini mwa.


WAZAZI WA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU

Asha Khamis mzazi wa mtoto mwenye ulemavu  wa akili kutoka Micheweni, amesema katika mkoa wao  wa kaskazini Pemba, skuli nyingi hazina walimu wa kufundisha elimu mjumuishi.

 ‘’Tunakilio kikubwa sisi wazazi kwani watoto wetu wenye ulemavu hawasomi, tunawaacha tu majumbani kwa sababu  hata  wakienda skuli, hawafahamu chochote kinachofundishwa wanakwenda wakicheza  hakuna walimu wenye taluma,’’ alieleza.

Khatibu Mjaja kutoka Kwale Micheweni alieleza kuwa, yeye mtoto wake anaulemavu mchanganyiko na ameshindwa kumpeleka skuli, kwani hakuna mwalimu anaeweza kuzungumza nae na wakaelewana.

‘’Naumia kuona mtoto wangu huyo anakosa haki yake ya elimu kwa sababu tu ya ulemavu wake, sasa sjui  Serikali  yetu  inampango  gani ya kuimarisha miundombinu ya elimu, ili kuona wanafunzi wenye ulemavu wanapata elimu,’’anasema.

 Mama mzazi wa mwanaunzi mwenye ulemavu wa viungo kutoka Kijichame Siwawi Omar, alisema kwa kweli  walimu wengi wanaofundisha maskulini hawana taaluma za kufundisha watoto wenye ulemavu.

‘’Ni vyema kuwepo na walimu wenye taluma ya kufundisha wanafunzi wenye ulemavu, kwani bila ya hivyo siku zote tutawaacha nyuma kimaendeleo,’’ alisema mzazi

‘njiani tu na ni kuwapa walimu mzigo tu’’ alieleza  mzazi.

WANAJAMII

Zahran Mohamed Yussuf mwanajamii kutoka Chake Chake ameeleza kuwa jamii iliokubwa ya watu wenye ulemavu wamekuwa wakikosa haki yao ya elimu na wamekuwa wakiachwa majumbani.

‘’Serikali watu wote ni wake na wote wanahitaji  haki sawa  hivyo tuikumbushe Serikali yetu  ya  Zanzibar kuweka mikakati  madhubuti  ikiwemo  kusomesha  kwa  wingi  walimu  mjumuishi  jambo  ambalo litapunguza manun’guniko,’’ alishauri.

Sambamba na hilo aliwataka wadau wanaoshughulikia watu wenye ulemavu kuongeza nguvu ya kuwasemea  na kuwatetea watu hao, ili kuona nawao wanapata fursa mbali mbali za kimaendeleo.

JUMUIA ZINAZOSHUHULIKIA WATU WENYE ULEMAVU

Kombo Ali Hamad Katibu wa jumuia ya watu wenye ulemavu wilaya ya Wete mkoa wa kasakazini Pemba, alisema  kwa kweli  walimu mjumuishi, maskulini ni kilio  kikubwa  kwa  wanafunzi  wenye ulemavu.

‘’Wanafunzi  wenye  ulemavu  wanahaki  ya  kupata  elimu  na  kuajiriwa lakini  waliowengi  wanakata  tamaa  hawafikii  ndoto  zao  kutokana na mazingira magumu yaliopo skulini,’’ alieleza

Amesema  kwa  sasa  elimu  mjumuishi  ni  jina  tu,  lakini  watu  wenye  ulemavu hawafaidiki  na   dhana   hiyo  kwani  vifaa vya  kufundishia  na  walimu wenye  taaluma  hiyo  hawako.

Mudathir Sharif Khamis Naibu Katibu katika Jumuia ya watu wenye uwalbino kisiwani Pemba, amesema licha ya mchakato mkubwa uliofanyika, ili kuwepo na elimu mjumuishi lakini bado  wanafunzi  wenye ulemavu, wanaendelea  kukumbwa  na changamoto.

‘’Katika wilaya yetu ya Chake chake kuna wazazi wamekua wakitoka Ndagoni, Wesha  na watoto wao wenye ulemavu  kuwapeleka  skuli ya Michakaini, ambapo ndio kituo kilichochaguliwa kitoe elimu mjumuishi, ni masafa marefu  na maisha yenyewe haya tulionayo,’’ alieleza .

 Hivyo ni lazima Serikali ikae itafakari hilo kwani mwisho wa  siku  kutawafanya wazazi hao  kuwakatisha watoto wao na kubaki nao majumbani mwao kutokana na lengo lao walilokusudia la kupata  haki yao ya elimu halifikiwi.

 Mratibu wa Jumuia ya watu wasiona [ZANAB] wilaya  ya  Chake  chake Suleiman Mansur, ameleza  kuwa  elimu mjumuisho bado haijawanufaisha wanafunzi wenye ulemavu, jambo ambalo linapelekea kufeli kwa masomo yao.

 ‘’Kuna baadhi ya walimu wanapewa taluma ya kufundisha elimu mjumuishi kwa muda wa miezi mitatu kwa kweli hiyo haitoshi, kama wanataka wenye ulemavu na wao wafaidike na elimu basi ni vyema somo la elimu mjumuishi,’’alieleza.

 Mratibu wa ZAPDD Kisiwani Pemba Khalfan Amour Mohamed, ameeleza kuwa bado waalimu waliowengi hawajakuwa na taaluma ya kuwafundisha wanafunzi wote wenye ulemavu kulingana na mahaitaji ya mwanafunzi mwenyewe.

‘’Bado ule ujuzi na uwelewa wa kuwafundisha wanafunzi wenye ulemavu, mfano wenye ulemavu wa akili, na Viziwi hawajakuwa nao wa kutosha,’’ alieleza khalfan.


WANAHARAKATI

Mwanaharakati kutoka chama cha wandishi wa habari Wanawake Tanzania Tamwa ofisi ya Pemba Fath-iya Mussa Said amesema suala la walimu wa elimu mjumuishi bado ni kidogo maskulini watoto  wenye ulemavu wanaendelea  kuteseka.

‘’Bado watoto wetu hawajapata walimu wa kuwasomesha mana mwalimu mmoja ana madarasa manne matano jee atakua na muda gani wa kuwafundisha wenye ulemavu na wakafahamu bado serikali hili ni tatizo la kuliangalia kwa upeo wa juu zaid’’ alieleza mwanaharakati.

WIZARA YA ELIMU

Mratibu wa Elimu mjumuisho na Stady za maisha ‘EMSM’ Pemba Halima Mohamed Khamis   amekiri  kuwepo kwa tatizo hilo la walimu  hususani waalimu wa kuwafundisha viziwi  pamoja na wasiona .

 

‘’Kwa kipindi cha mwaka jana  tulikua   tuna idadi ya wanafunzi  wenye ulemavu 1710   lakini  ukiangalia  walimu  wote waliosomea elimu mjumuishi ni  69  ndani ya Pemba, hivyo bado shida ipo  ukiangalia na idadi ya wanafunzi tulionao’’, alisema  Mratib.

Aidha amesema Serikali kwa kuwajali wanafunzi  wenye ulemavu tayari imeshachukua  idadi ya walimu   watakaofundisha  elimu mjumuishi kwa ajili ya kuwajiri   ili kuondosha tatizo  hilo kwa wanafunzi wenye uhitaji maalum.

 

KATIBA YA ZANZIBAR

Kifungu cha [10] [g] kinafafanua kwamba Serikali itawekea mazingira rafiki kwa makundi ya wagonjwa, waliojiajiri, Wazee, Watoto na watu wenye ulemavu.

Lakini hata kifungu cha 12 [1] kimesema  kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.

Sheria ya watu wenye ulemavu sheria namba 6 ya mwaka 2022 kifungu cha 28 [1] kimesema kuwa watu wenye ulemavu wanastahiki haki zote za msingi za binadamu sawa na watu wengine ikijumuisha, haki ya elimu, ikijumuisha mafunzo ya amali na mafunzo ya kukabiliana na maisha kulingana na aina za ulemavu.

Pia kifungu kidogo cha [2] kimesema kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha kwanza [1] [a] cha kifungu hiki, Baraza kwa kushirikiana na taasisi yenye dhamana na masuala ya elimu itahakikisha; watu wenye ulemavu wanapata elimu na mafunzo ya amali katika ngazi zote na kuwepo na mfumo wa elimu mjumuishi unaozingatia mahitaji maalum ya watu wenye ulemavu katika ngazi zote za elimu.


Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.