WASAIDIZI WA SHERIA PEMBA WAPEWA MBINU JUU YA KUPAMBANA NA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA.
Wasaidizi wa
sheria wamehimizwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuona wanakuwa na
uthubutu wa kwenda mahakamani kutoa ushahidi pamoja na kuripoti vituo vya
Polisi wakati kesi zitakapotokezea.
Hayo
yamesemwa na Kamanda wa polisi mkoa wa Kusini Pemba Richad Mchovu wakati
akifungua kongamano la kutimia kwa miaka 10 yautoaji wa huduma wa msaada wa kisheria [Lsf]huko Skuli ya
Michakaini Chake chake Pemba.
Amesema
wasaidizi wa sheria wamekua wakifanya kazi kubwa ya kuibua na kuyaripoti
matendo ya udhalilishaji lakini bado jamii inaonekana imegubikwa na tatizo la
rushwa muhali.
Hivyo
amewataka wasaidizi wa sheria kuongeza jitihada ya kuwailimisha wanajamii
madhara ya rushwa muhali pamoja na kuwajengea uwezo wa kusimama mahakamani
jambo ambalo lisaidia kuondokana na udhalilishaji wa Wanawake na watoto.
Kamanda huyo
ameahidi kutoa mashirikiano ya hali ya juu kwa wasaidizi wa sheria pamoja na
ulinzi shirikishi katika mapambano dhidi ya udhalilishaji ili kuona
wanawadhibiti wanaofanya makosa hayo na kuona kesi hizo zimepatiwa ufumbuzi.
Mapema kaimu
mratibu wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar ofisi ya Pemba Safia Saleh
Sultan amesema bado jeshi la polisi linaonekana halijakua tayari katika
mapambano dhidi ya udhalilishaji, hivyo basi wakati umefika kuona tasisi zote pamoja
na wanaharakati kushirikiana kwa pamoja na kua na kauli ya pamoja ili kuona
kila mmoja anatekeleza wajibu wake kwa kuzingatia madili ya kazi yake.
Comments
Post a Comment