WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KATIKA VIYUO VYA AFYA KUCHOMA CHANJO YA UV19
NA FATMA
HAMAD FAKI.
Wananchi
wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika vituo vya afya kuchoma chanjo ya uviko
19 ili waweze kujikinga na ugonjwa huo.
Wito huo
umetolewa na mratibu wa chanjo Kisiwani Pemba Bakar Hamad Bakati wakati
akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika zoezi la uchanjaji wa chazo
hizo, kwa wananchi wa shehia ya Sizini wilaya Micheweni Mkoa wa Kaskazini
Pemba.
Alisema
kinga ni bora kuliko tiba, hivyo ni vyema kila mmoja kuhakikisha amechoma
chanjo ya uviko 19 jambo ambalo litaepusha kuenea kwa ugongwa huo katika jamii.
Alisema
chanjo hiyo itaendelea kutolewa katika kituo cha Afya cha sizini, hivyo
wananchi wajitokeze kwa wingi kituoni hapo na kupatiwa chanjo.
‘’Tumeamua
kuleta chanjo katika kituo hicho jambo ambalo liwarahisishia wananchi kufuata
masafa ya mbali huduma hiyo’’ Alisema mratibu Bakari.
Aidha
amefahamisha kuwa wanaostahiki kupata chanjo hiyo ni watu wa zima kuanzia umri wa miaka
18,wakiwemo na wajawazito.
Baadhi ya
wananchi hao wamesema wataendelea kuhamasishana ili kuhakikisha kila mmoja
amechoma chanzo hiyo katika kijiji chao.
Huduma hiyo
inaendelea kutolewa katika vituo vya afya vilivochagulia ikewemo konde
micheweni na wingwi pia inatolewa vijijini kupitia hduma za mkoba.
Comments
Post a Comment