WANANCHI WATAKIWA KUIDUMISHANI AMANI


 Wananchi wametakiwa kuendelea kuutunza Umoja  na mshikamano uliopo  sasa ili  kuona Amani imetawala na nchi inapinga hatua katika nyanja mbali mbali za  kimaendeleo.

Akizungumza na watendaji wa azaki za kiraia Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Masoud wakati akifungua kongamono la kumpongeza Rais mwinyi kwa kipindi cha mwaka mmoja alichokaa madarakani lililofanyika ukumbi wa baraza mji Chake chake Pemba.

Alisema suala la kutunza Umoja ni jukumu la kila mtu, hivyo ni vyema kila mmoja kwa nafasi yake kuendeleza umoja huo ili kuona hakuna vitendo vyovyote viovu vinavyojitokeza.

‘’Nawasihi wananchi tuutunzeni umoja wetu na mshikamano wetu ili tuweze kufanya kazi zetu kwa uhuru’’ alisema Mattar.

Alisema bila ya kuepo kwa amani si rahisi kupatikana kwa maendeleo, hivyo  aliitaka Jamii kujiepusha kufanya vitendo viovu ambavyo vinaashiria uvunjifu wa amani.

Alisema Rais Mwinyi kwa kuwajali Wananchi wake  ndio akamua kuunda umoja wa kitaifa ili kuwaunganisha Wazanzibar wote kuwa kitu kimoja bila ya ubaguzi wowote.

Aidha alifahamisha kuwa tokea kukaa kwake madarakani Rais Mwinyi kumeanzishwa miradi mbali mbali ya kimaendeleo  nchini ambayo italeta manufaa kwa Wananchi pamoja na Taifa.

Mapema mratibu wa tumaini jipya [TUJIPE] Pemba Tatu Abdala Mselemu alisema katika utawala wa dk  Mwinyi Asasi za kiraia zimepata mafanikio makubwa kwani zimeweza kutambulika zaidi katika mpango wa Sera,  Sheria na mipango ya kimaendeleo.

Aidha alieleza kuwa kwa sasa asasi za kirai zimepata fursa kubwa ya kutekeleza shuhuli zake  mbali mbali za kimaendeleo bila ya kuwekewa vizuizi vyovyote.

Kwa upande Hidaya Mjaka Ali  kutoka jumuia ya watu wenye ulemavu, amempongeza Rais Mwinyi kwa kuanzisha mahakama maalumu inayosikiliza kesi za udhalilishaji jambo ambalo  tasaidia kupatiwa ufumbuzi  kwa haraka kesi za watu hao.

Kongamano hilo limeandaliwa  na mtandao wa asasi za kiraia [ PACSO] ambapo ujumbe wa kongamano hilo unasema  Neema ya Amani na Umoja wetu, safari ya ujenzi wa Uchumi mpya inaendelea’.



Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.