HATIMAE MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO MWENYE ULEMAVU WA KIUNGO APATIWA MSAADA.
NA FATMA HAMAD FAKI,PEMBA
Hatimae
Wahisani na wafadhili wameanza kujitokeza kumsaidia kijana Anifu
Jeilani Isaa mwenye ulemavu wa viungo,
mwanafunzi wa darasa la tano katika skuli ya msingi Ole ambae ilikua anakabiliwa na changamoto ya
baskeli ya maringi mawili kwa ajili ya kwendea skuli.
Akikabidhi msaada huo Katibu wa CCM Jimbo la
Ole Yakoub Khalfani Shaha kwa niaba ya Mwakilishi wa Jimbo hilo ambaye pia ni
Waziri wa nchi Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum
za SMZ Masoud Ali Mohd ,alisema msaada huo umekuja baada ya kuona taarifa
zilizo rushwa kwenye mitandao ya kijamii juu ya shida inayo mkabili kijana huyo
iliyosababisha kukatisha masomo yake.
‘’Baada ya taarifa zilizo samba mitandaoni
juu ya shida zilizokuwa zikimkabili kijana huyo tumeamua kumsaidia ili
aondokanae na kero hizo’’ alisema katibu huyo.
Akitoa shukrani za dhati Mama mkubwa wa mtoto
huyo Fatma Moh’d Omar mara baada ya kupatiwa msaada kwa kijana wake huyo alisema
kuwa utaweza kumsaidia kutafuta haki yake ya msingi ya elimu huku akimshauri mwakilishi
huyo kuendelea kumsadia.
Aidha bi Khadija aliwataka wazazi wenye
watoto walemavu kuacha tabia ya kuwafungia majumbani na badala yake wawapeleke
Skuli pamoja na madrasa ili waweze
kujipatia haki yao ya elimu.
Comments
Post a Comment