JAMII YATAKIWA KUSIMAMA KIDETE KUKOMESHA UDHALILISHA WA KIJINSIA

Afisa Mdhamini Ofisi ya Raisi tawala za mikoa Serikali za mitaa  na idara maalumu SMZ Thabiti Othmani Abdalla ameitaka Jamii kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya matendo ya udhalilishaji yanayoendelea kujitokeza siku hadi siku hapa nchini.

Ushauri huo ameutoa wakati akizungumza na wanafunzi wa Vyuo mbali mbali Kisiwani Pemba huko katika kituo cha huduma za Sheria ikiwa ni shamra shamra za kuelekea katika maadhimisho ya siku 16 ya kupinga matendo ya udhalilishaji.

Amesema Kila mtu anapaswa kuunga mkono juhudi za serikali katika kupinga matendo ya udhalilishaji.

Amesema wakati umefika kwa jamii kuacha muhali na kusimama mahakamani kutoa ushahidi katika kesi hizo ili kuona zinafikia hatua inayostahiki


.Kwa upande wake Mratib wa Kituo cha Huduma za Sheria Pemba,Safia Seleh Sultan amewaomba wanafunzi hao kuzisoma sheria ambazo zitaweza kuwasadia na kuwalinda katika mapambano dhidi ya  Vitendo vya  udhalilishaji.

Nao washiriki wa mkutano huo wameitaka Serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa wale wote watakaobainika wakizifanyia suluhu majumbani kesi za udhalilishaji pamoja na wale wote wanaowatorosha wafanyaji wa makosa hayo

Mkutano huo ni moja ya shamra shamra ya madhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia.

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.