UTELEKEZAJI BADO NI TATIZO KWA WANAWAKE NA WATOTO
Utelekezwaji wa wanawake na watoto ni moja ya sababu inayopelekea kuongezeka kwa matendo ya udhalilishaji katika Jamii.
Akizungumza
na wandishi wa habari huko ofisini kwake mratibu wa jumuia ya Tumaini Jipya [TUJIPE] Tatu Abdala
Mselem amesema imebainika kuwa watoto wengi wanaotelekezwa na wazazi wao hujiingiza
katika masuala ya omba omba na kupelekea
kufanyiwa udhalilishaji.
Aidha
alifahamisha kuwa akina baba wengi wanapoachana na wenzao wao hawatowi matunzo
ipasavyo kwa watoto wao na kupelekea kukosa
haki zao za msingi.
‘’Wazazi
wanapoachana watoto huathirika zaid kwani huwa ni sababu ya wao kutelekezwa na
kukosa matunzo’’ alisema Bi tatu.
Mapema
makamo mwenyekiti wa tumaini jipya Suleimana Mohd Iddi alisema licha vitendo
hivyo vikionekana kujitokeza kila siku lakini
bado jamii imekua ikiyafumbia macho matendo hayo na kufanya suluhu
majumbani wakidai wanaogopa ugomvi
kwenye familia zao.
Jumjla ya majalada 107 ya kesi za udhalilishaji yalipokelewa katika ofisi ya mkurugenzi wa Mashtaka [DPP] kuanzia January hadi Novemba mwaka huu, majalada 64 yalipelekwa mahakamani, 15 yalirejeshwa kwa upelelezi, 11 yalifungwa, 9 yalimaliza, 5 waliachiwa huru na 3 yaliondolewa.
Comments
Post a Comment