WADAU MBALI MBALI WASHAURIWA KUSHIRIKIANA KWA PAMOJA ILI KUMALIZA UDHALILISHAJI.
NA FATMA HAMAD PEMBA. Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mheshimiwa Matar Zahor Massoud amesema Kuna ulazima wa kila mdau kushiriki kwa pamoja katika kusimamia Sheria na kanuni za kesi za udhalilishaji Ili kuiokoa Jamii kuondokana na majanga ya ukatili na udhalilishaji nchini Akizungumza kwa niaba ya Mkuu huyo wa Mkoa , Mkuu wa Wilaya ya Wete Dr Hamad Omar Bakar huko uwanja wa Mshaame Mata Micheweni katika maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia yaliyoandaliwa na Jumuiya inayopingana na ukatili na udhalilishaji wa kijinsia TUJIPE amesema udhalilishaji umekuwa kikwazo Cha kuleta maendeleo kwa wanawake na watoto hivyo Ili kuisaidia juhudi za Taifa katika kutokomeza janga Hilo ni budi kwa kila mmoja kuendelea kusimamia jukumu alilopangiwa Mapema mratibu wa jumuiya inayopingana na ukatili na udhalili Shaji wa kijinsia ya Tumaini Jipya (TUJIPE) Tatu Abdallah Mselem amesema licha kuwepo kwa Sheria na hukumu zinazotokewa katika watendaji wa matendo hayo Bado udhalilishaji unaendelea hivyo Kila mdau wa mapambano hayo anapaswa kuchukua hatua kwa nafasi yake Naye mlezi wa TUJI PE ambaye pia ni mdhamini wa Afisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Thabiti Othman Abdalla ameitaka Jamii na viongozi wengine kuacha muhali na kusimama imara katika kukabiliana na janga Hilo Ili kuisaidia Serikali na Jamii kuondokana na matendo ya ukatili na udhalilishaji nchini |
Comments
Post a Comment