MUHALI BADO NI TATIZO KATIKA KESI ZA UDHALILISHAJI
NA FATMA HAMAD PEMBA.
Ushiriki
mdogo wa wanajamii dhidi ya utoaji wa ushahidi mahakamani bado ni changamoto kubwa inayopelekea kesi za udhalilishaji kushindwa kupata hatia jambo ambalo
linachangia kuongezeka kwa vitendo hivyo.
Akizungumza
kwa dharura ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya mkoani Khatib Juma Mjaja amesema
ni muhimu kwa vilabu vya mazoezi kushirikiana na wanaharakati mbali mbali
kuielimisha jamii kujua madhara ya rushwa muhali kwani ni adui katika mapambano
hayo.
Aidha
ameahidi ushikiano sambamba na kuomba umoja huo kuandaa mbinu madhubuti ya
kuibua na kuyaripoti matendo hayo ili kuhakikisha wafanyaji wa matukio hayo
wanapatikana na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
‘’Sasa ni
wakati wa kutekeleza kwa vitendo, hivyo ni jukumu la kila mmoja kusimama kwa
nafasi yake kuunga mkono juhudi za kupinga
tatizo hili ambalo limekua ni kilio
kwa wakaazi wa Zazibar’’ alisema mkuu wa wilaya.
Awali
akisoma risala mjumbe kutoka umoja wa vilabu vya mazoezi ya viungo Pemba Shaame Farahani Khamis amesema lengo la
bonanza hilo ni kuunga mkono juhudi za Serikali kwani bado changamoto ni nyingi
na matendo yanaongezeka hali inayorejeshanyuma vita dhidi ya udhalilishaji na ukatili wa wanawake
na watoto.
Amesema
miongoni mwa changamoto hizo nipamoja na rushwa muhali na kuepo kwa baadhi ya viongozi wasio
waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao.
Nae
mkurugenzi wa chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania [ TAMWA- Zanzibar
] Mzuri Issa Ali ameliomba jeshi la
polisi pamoja na mahkama kuunga mkono juhudi hizo kwa vitendo kwani kesi nyingi zinafeli hazipatiwi hukumu
kwa kisingizio cha kukosekana kwa ushahidi.
Bonanza la
umoja wa vilabu vya maazoezi ya viongo pemba ni miongoni mwa maadhimisho ya
kilele cha siku 16 za kupinga udhalilishaji sambamba na uzinduzi wa umoja huo
ambapo jumla ya vilabu 17 vimeshiriki kutoka sehemu tofauti kisiwani Pemba.
Comments
Post a Comment