WAZAZI WAOMBWA KULEA WATOTO WAO KATIKA MALEZI YA PAMOJA
Hayo yamesemwa na kaimu mratibu wa kituo cha
huduma za sheria Safia Saleh Sultan
wakati akizungumza na wanakikundi cha chapa kazi cha wanakisomo kilichopo Kwale Gombani Chake chake Pemba.
Alisema
kukosekana kwa kizazi chenye madili ni moja ya sababu inayopelekea kuongezeka
kwa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, hivyo wakati umefika kwa wazazi
kushirikiana kwa pamoja ili kupunguza tatizo hilo hapa nchini.
Akiwasilisha mada katika mkutano huo Khadija kutoka
kituo cha huduma za sheria amewataka
wazazi fuatilia nyenendo za watoto wao wakati wanapokwenda skuli na
madrasa ili kuwalinda na vitendo viovu vikiwemo vya udhalilishaji.
Samba mba na
hilo amesema endapo jamii itatoa huduma stahiki kwa family zao inaweza
ikasaidia watoto kujiepusha kujitumbwikiza katika vigenge viovu ambavyo
vinachangia kwa kiasi kikubwa wimbi la udhalilishaji.
Comments
Post a Comment