ATIWA MBARONI AKIDAIWA KUMLAWITI MLEMAVU WA AKILI

Msifunzwa ni mamae hufunzwa ni ulimwengu  hii imekuja baada ya Nuhu Kombo Nuhu mwenye mumri wa miaka 22  akihemea polisi kwa tuhuma za kumlawiti kijana  wa 18 mwenye ulemavu wa akili na mdomo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mama mzazi wa kijana huyo amesema ailikua yupo nae nyumbani badae akatoka  na hakurudi tena  na alianza kumtafuta ila hakumuona.

Alisema kuwa baada ya muda   mrefu kupita  aliletewa   nyumbani  na msamaria mwema na kumuambia huyu mtoto wako nimemkuta  Vichakani akiwa anafanyiwa udhalilishaji na Nuhu Kombo Nuhu.

Alifahamisha  kuwa  baada ya hapo aliendelea kumuhoji na kumuambia kuwa hii ni kawaida yake kumchukua na kumpeleka vichakani  kumfanyia kitendo hicho

‘’Nilipo muhoji aliniambia ashazoea kunifanyia hivi  na ananiambia atanipa pesa na simu ya tachi’’ alieleza mama mzazi.

Aidha mama huyo alisema kuwa baadhi ya wanafamili wa mtuhumiwa huyo wamekua  wakimtolea maneno mabaya huku wakimtaka  wafanye suluhu ili kesi isiendelee.

‘’Kitendo hicho cha kinyama alichofanyiwa mwanangu nimekipokea kwa masikitiko makubwa kutokana na hali ya mwanangu  kwani hana akili na hasemi, hivyo siko tayari na suluhu nitasimama kidete mpaka haki itendeke’’ alieleza mama mazazi.

Hivyo aliviomba vyombo vinavyohusika kutoa adhabu kali kwa muhalifu huyo ili iwe dawa kwa wengine.

Sheha wa shehia ya Sizini Nassor Kombo Khator alisema kitendo hicho cha kinyama kimemuhuzunisha hivyo amewaomba wazazi na walezi kuwa karibu zaid na watoto kwani   udhalilishaji  umeenea kila sehemu.

Aidha aliwashauri wanajamii kuondosha muhali na kuwa na ujasiri wa kuyafichua na kuyaripoti matendo haya katika vyombo vya sheria jambo ambalo litapunguza  masuala haya.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kaskazini Pemba Juma Sadi Khamis alisema tukio hilo limetokea siku ya jumatatu  tarehe 13 mwezi huu ambapo alimlawiti na  kumsababishia maumivu na kwasasa mtuhumiwa yupo kituo cha polisi Micheweni.

Sambamba na hilo kamanda alisema vitendo vya udhalilisha vimeshamiri  hivyo wakati umefika kwa wazazi kuka na watoto wao na kuwaelimisha juu ya madhara ya udhalilishaji jambo ambalo litawafanya kuwa na woga juu ya masuala hayo.

Nae afisa kutoka jumuia ya watu wenye ulemavu wa akili kisiwani Pemba  [ZAPPDD]   Khalfan  Amour  Mohd amelaani kitendo hicho kwani ni aibu kwa kijana mwenyewe na hata kwa Taifa.

Amesema kila mmoja ni mlemavu mtarajiwa hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuwalinda watu hao ili kuwaepusha na udhalilishaji .

Hivyo amesema  watahakikisha wanaifuatilia kesi hiyo mpaka haki ya kijana huyo ipatikane.



 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.