WAZAZI WATAKIWA KUTOA MATUNZO STAHIKI KWA FAMILIA ZAO
Wazazi na
walezi wamehimzwa kuendelea kutoa huduma stahiki kwa watoto wao jambo ambalo
litaepusha kufanyiwa kwa udhalilishaji
wa kijinsia kwa watoto.
Ushauri huo
umetolewa na Siti Habibu Mohd kutoka kituo cha huduma za Sheria ofisi ya Pemba
wakati akitoa elimu juu ya kuripoti matendo ya udhalilishaji kwa wanafunzi wa Skuli ya Madungu Msingi
alisema bado suala la udhalilishaji linaendelea kufanyika kila siku , hivyo ni
vyema wazazi kuwa na ukaribu wa hali ya juu pamoja na kuwapatia huduma ili kuwalinda na vitendo hivyo.
‘’Nawasihi
wazazi wenzangu tujitahidi kuwahudumia watoto wetu ili tuwalinde na vitendo
viovu’’ alisema Bi siti.
Sambamba na hilo aliwataka wanajamii kushirikiana na vyombo vya kisheria kwa kuwafichua watendaji wa makosa hayo pamoja na kutoa ushahidi mahakamani jambo ambalo litapunguza matendo hayo.
Aidha aliwataka wanafunzi hao kutoa tarifa kwa watu wao wa karibu ikiwa ni pamoja na wazazi, walimu wao, wakati wanapofanyiwa vitendo vya udhalilishaji ili kujinusuru na janga hilo.
‘’Udhalilishaji
unafanyika kila eneo hivyo tumeamua kuwapa elimu wanafunzi hawa ili wawe na
uthubu wa kuyaripoti.
Alisema bado
kuna watoto wamekuwa wakifanyiwa vitendo hivyo lakini hawana uthubutu wa kuyaripoti katika sehemu
husika na kupelea kuendela siku hadi siku.
Alisema
lengo la kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi hao ni shamra shamra maadhimisho ya
siku 16 ya kupinga udhalilishaji wa kijinsia.
Comments
Post a Comment