JAMII YAHIMIZWA KUWATUNZA NA KUWATHAMINI WATU WENYE ULEMAVU.


 kikundi  Cha Mazoezi  ya viungo cha Gombani Fitnes Senter  kilichopo chake chake  kimemtembelea   na kumfariji kijana Asaa Khamis mwenye ulemavu  wa Viungo Mkaazi wa Shumba ya Vyamboni  wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba  kufuatia   habari iliyorushwa katika Blog ya Pemba ya leo    iliyo muhusu kijana huyo  akihitaji msaada  wa kupatiwa mtaji  kwa  ajili ya kuendeleza biashara zake.

Akizungumza mara bada ya kumfariji kijana huyo  katibu wa Kikundi  hicho  Khalfan Amour  Mohd alisema mbali ya kukindi hicho kufanya mazoezi  pia kimekua kikifanya harakati mbali mbali za kijamii kama vile kusaidia watu wenye ulemavu, pamoja na kupiga vita masuala ya udhalilishaji hususan kwa walemavu .

‘’Unajua sisi tumeguswa na makala iliyorushwa kwenye mtandao inayomzungumzia Kijana Asaa jinsi anavyopata shida kutokana na ulemavu wake tukaona ipo haja kumfariji kwa vile na sisi ni walemavu watarajiwa’’alisema Khalfani.

Alisema watu wenye ulemavu wanakumbana na changamoto nyingi katika maisha yao hivyo ipo haja kuangaliwa, na kushirikishwa katika fursa mbali mbali za kimaendeleo.

Hata hivyo katibu huyo aliviomba vikundi vyengine vya mazoezi kuiga mfano huo wa kusadia makundi maalumu na hata harakati nyengine za kijamii.

Akitoa shukurani kijana asaa baada ya kupokea msaada  kutoka kwa wana michezo hao alisema jambo walilolifanya ni  la historia kwake  huku akiwaomba waendelee na imani hiyo hiyo ya kusaidia kwani ujira wao wataona kesho mbele ya Allah  [SW].

 


Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.