UMOJA WA VILABU UNAWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KATIKA MADHIMISHO YA SIKU 16 YA KUPINGA UDHALILISHAJI
Akizungumza na wandishi wa habari katika ofisi za
Tamwa Mkanjuni Chake chake katibu wa jumuia ya umoja wa vilabu vya mazoezi
kisiwani Pemba Khalfan Amour Mohd alisema
umoja huo umeamua kuadhimisha siku hiyo ili kuunga mkono juhudi za
Serikali katika mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake na watoto ambao umekua
ukiwakumba mara kwa mara katika jamii.
Alisema kumekuwepo na vitendo vingi vya ukatili wa
kijinsia ambavyo huakumba zaid Wanawake na watoto, hivyo wameona ipo haja nawao
kuchukua jitihada za makusudi za kuzipigia
kelele zile kero ambazo zinawakumba wanawake na watoto katika jamii na
kuzifikisha katika mamlaka husika ili kuona haki inatendeka.
‘’Tumeona kwa vitendo vya udhalilishaji
vinafanyika katika jamii zetu tunazoishi, hivyo tumeamua na sisi tujitolee na
tuweze kushirikiana na wadau mbali mbali kupiga vita vitendo hivy’’ alisema
katibu.
Alisema ili
kupunguza tatizo hili hapa Nchini ni vyema kila mmoja kwa nafasi yake kuchukua
hatua ipasavyo pamoja na kufanya kazi zao kwa uadilifu kwa misingi ya sheria na
nidhamu.
Aidha ameipongeza Serikali ya mapinduzi ya
Zanzibar kwa kuweka mikakati mbali mbali
ili kuona kesi hizi zinaendeshwa kwa haraka na kupatiwa hukumu.
Comments
Post a Comment