MAHAKIMU NA MAJAJI WAHIMIZWA UWADILIFU KWENNYE KUTOA HAKI

 

NA FATMA HAMAD, PEMBA

Watendaji wa Mahakama kisiwani Pemba wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu zaidi ili kuhakikisha Wananchi wote wanapata haki zao bila ubaguzi.

Hayo yamesemwa na Mrajis wa mahakama Zanzibar Valentina Andrew Catema wakati akizungumza na wafanyakazi wa Mahakama mkoa wa   wa Kaskazini Pemba.

Amesema suala la utoaji wa haki ni kipengele muhimu katika uendeshaji wa kesi, hivyo wanadhima kubwa ya kuhakikisha wanafanya kazi bila ya ubaguzi jambo ambalo litasaidia wananchi kujenga imani na Mahakama.

‘’Niwambie ndugu zangu mnadhima kubwa kwa jamii, hivyo fanyeni kazi kwa umakini ili kuhakikisha mnatenda haki,alisema.

Aidha aliwataka watendaji hao kudumisha umoja na mshikamano wao katika utendaji wa majukumu yao, kwani kufanya hivyo kutawawezesha kufanya kazi  kwa ufanisi wa hali ya juu.

 

Kwa upande wake hakimu dhamana wa Mahakama ya Mkoa Wete Mumin Ali Juma alisema licha ya mafanikio makubwa waliofikia lakini bado wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa Fedha za kuwalipa mashahidi, jambo linalosababisha wengi wao kushindwa kufika Mahakamani na kutoa ushahidi.

,,Tuna kilio Mheshimiwa Jaji tunapata pesa kidogo za kuwalipa mashahidi wetu, hali ambayo inapelekea kuwa na deni kubwa za mashahidi, alieleza.

Mapema Jaji mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdala aliwataka wafanya kazi hao kuendeleza kutekeleza majukumu yao licha ya vikwazo vinavyo wakabili, huku akiahidi kuzifanyia kazi na kuhakikisha zimetatuliwa ili waweze kufanya kazi katika mazingira rafiki.

 Nao wafanya kazi hao walimtaka Jaji huo kuboresha maslahi ya wafanya kazi wa Mahakama za Pemba wafanye kazi zao kwa ufanisi zaidi


Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.