UCHUMI MDOGO ULIMFANYA MWANAMKE AWE KIONGOZI

 

NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR

Binaadamu siku zote hutakiwa ajuwe alipo na wapi anataka kwenda. Katika maisha hii huwa ni ndoto ambayo humpelekea mtu kupitia mengi, baadhi yao yakiwa ni mtihani mmoja baada ya mwengine.

Jambo muhimu ni kutokata tamaa na kuendelea kupambana na pale unapoteleza au kuanguka unapaswa kuinuka na kuendelea na safari huku ukiwa na matumaini ya siku moja utafika huko unapokusudia kwenda.

Bi Huzaima  Ali Hamdani, miaka 51, ambae ni mjasiria mali wa uchoraji piko  na biashara ya vyakula, ni mmoja wa wanawake aliyekabiliana na mithani mingi katika safari yake ya uchoraji aliyoianza 1997.

Kila alipokutana na kikwazo hakukata tamaa, bali aliendelea kupambanana na  kuanza biashara nyengine, ikiwemo ya kuuza urojo, maandazi na chapati, ili kuhakikisha anajipatia kipato cha halali cha kujiendesha kimaisha.

"Kila siku asubuhi nauza urojo, mandazi chapati na juisi na ikifika jioni nauza supu ya utumbo na chapati,"alisema.

Alipomsikia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, akisema wachoraji watapewa mfuko wa kuendeleza biashara zao hakusita kufuatilia kwa kwenda halimashauri kujaza fomu ambayo imeshafikishwa benki na anayo matumaini  ya kupata mkopo utakaomsaidia kuimarisha biashara yake.

Wakati akiendesha biashara zake alikuwa ameshajiunga katika Chama cha Democrasia na Maendeleo ( Chadema) akiwa mwanachama katika mwaka 1996 na baada ya muda alichaguliwa kuwa kiongozi katika tawi.

Wazazi wake walimuwekea pingamizi hapo awali, lakini hilo halikumkatisha tamaa kwa vile alikuwa na ndoto ya kuwa kiongozi na alifarajika alipoona mume wake hakuwa na pingamizi na akawa karibu naye.

Alipokuwa kiongozi katika tawi akawa bado hakuridhika na nafasi hio na akaingia katika kinyang’anyiro cha kugombea ubunge katika mwaka 2020 na ingawa hakubahatika kuipata nafasi hio hakukata tamaa na kuamini ipo siku ndoto yake itatimia.

Kisha alifanikiwa kuweka mikutano na anashukuru hakuanguka sana kwani alibahatika kupata kura 400, ambazo hazikumtosha.

"Nimeamuakuzikuzishabiasharazangupamojanavikundivyangukwalengolakuwezakunisaidiakatikaharakatizanguzakugombaniaubungenanikafanikiwakuchukuwafomu,nakuwekamikutanonanashukurusikuangukasananikabahatikakupatakura400ilanaaminimwakaninitapata."anaeleza

SABABU ZA KUINGIA KATIKA SIASA

Miongoni mwa mambo yaliyomsukuma kuingia katika siasa ni kutaka kusaidia kutataua matatizo wanayokutana nayo wanawanawake katika maisha ya kila siku. Hii ni pamoja na huduma duni za matibabu.

"Hadi leo ukienda katika hosptali kitanda cha wajawazito kimoja wanakaa watu watatu. Hili jambo linanikera na nimeamua nikiwa kiongozi mwenye nafasi ya kusaidia kulitatua nitasimama kidete kuhakikisha usumbufu huu unaondoka’’, alieleza.

Licha ya kutopata nafasi ya kuwa mbunge mwana mama huyu anaendelea kuongoza wenzake kwa kutoa elimu kwa wanawake wenzake ya kujitambua na kujuwa kwamba wanayo haki ya kuwa viongozi.

Pamoja na hayo anashirikiana na vijana na kuwasaidia anapokuwa na uwezo. Mfano mmoja ni wa kuona vijana wanashiriki katika michezo na aliwashaijisha vijana wa  wa jimbo la Welezo shehia ya Mchokichini, kwa kuwapelekea mipira na kuwafahamisha umuhimu wa kujihusisha na siasa kwa vile ndio msingi wa maisha yao ya kila siku, pamoja na kupeleka siasa katika kijiji cha tumbatu.

"NilipoendaTumbatuwaliniombaniwapatieofsinakwavileuwezowangubadonimdogo,nilichanganakuwapelekeashilingi300,000zilizosaidiamatengenezoyaofsihiyo,ingawamwishowasikuhawakunishikamkonokatikasafariyanguyakutakakusongambelekwenyeuongozi.Hatahivyosijakatatamaa,"aliongeza.

Miongoni mwa mafanikio ya harakati zake za kuongoza wenzake Bi Huzaima ameweza kuwashawishi  wanawake 10 kuingia katika uongozi.

"Baadayakuonasiasainakujenga,siasainamanufaanikamuwakuwashajihishawanawakewenzangunanikabahatikawanawake10kutakakuingiakatikauwongozinariskiikawangukiawanawakewawililakinihawakuvunjiakamoyowanaendeleakupambana."alisema

Alisema uzoefu alioupata ni unapofanya kazi kwa bidi wanatokea wenzako wanaokuwa hawafurahii na hukuona kuwa ni mtu unayejiona badala ya kuthamini kile unachokifanya.

Alieleza kusikitishwa kwake na kuona bado jamii inatawaliwa na mifumo dume ambayo humtenga mwanamke na hata kumuona hana haki ya kuingia kwenye safu ya uongozi na miongoni mwa wenye kufanya hivyo ni wanandoa.

"Lakini pia wapo wanawake ambao wamejijengea hofu ya kuingia kwenye siasa kutokana na kuwa na uelewa mdogo na kuona siasa ni kwa ajili ya wanaume pekee yao,’’alieleza.

 MAFANIKIO

Miongoni mwa mafanaikio aliyoyapata ni kujifunza mengi kupitia siasa na kuwa mtu anayejiamini na kuwa na ujasiri wa kuweza kuzungumza pahala popote.

Neema Saidi Mwishehe ambae ni mjumbe wa Baraza Kuu la  Taifa kupitia Chadema alikuwa mjasiria mali wa vyakula na kabla ya kuingia katika siasa alikuwa anauza urojo na wakati huo aliwaona wanachama wa Chadema walivyokuwa wanawahamasisha watu. Hapo ndipo  alipohamasika na kujikuta anaingia kwenye siasa katika mwaka 2018 wakati akiwa kijana mbichi wa miaka 18.

Alipojiunga na chama hicho alianza kutumikia nafasi mbalimbali, ikiwemo ya Mwenyekiti wa Shehia ya Kijitoupele na Mwenyekiti wa jimbo kwa upande wa vijana na baaadaye Mwenyekiti wa Wilaya hadi kufikia mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la chama hicho.

Akiwa katika nafasi hizo aliamua kuachana na biashara zake kutokana na a majukumu kuongezeka huku akiwa na shauku ya kujiendeleza kwenye  elimu na siasa.

Alisema miongoni mwa  watu waliomshajihisha kuingia katika siasa ni Huzaima ambae alimulewa kuwa ni mwanamke jasiri, anaejiamni na kuwajibika katika uongozi wake na hali hio ilimpeleeka  kumfanya mmoja wa watu waliokuwa wanampa ushauri.

Hata hivyo,  safari yake ya uongozi haikuwa nyepesi kwani alikumbana na  vikwazo ambavyo wanawake wengi hukutana navyo katika siasa, hasa wale wenye umri mdogo na alipata shida kuwaongoza watu waliomzidi umri.

Alisema miongoni mwa faida aliyoipata katika  chama chake ni elimu ya kupiga vita vitendo vya ukatili na udhalilishaji kwa wananchi na kumepelekea kuwa mstari wa mbele katika mapambano ya kutokomeza vitendo hivyo.

Hivi sasa anajitayarisha kugombania uwakilishi katika jimbo la Kijitoupele kupitia tiketi ya chama chake.

Asiata Said Abdala ambae ni mueka hazina wa Kanda ya Unguja katika CHADEMA alisema aligombea nafasi mbalimbali baada ya kushawishiwa na Huzaima ambaye alimuona kuwa ni mwanamke anayependelea maendeleo kwa wanawake wenzake.

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Shukuru Malonda, alisema mwanamke ana nafasi ya uongozi katika kanisa na kijamii na kutoa mfano wa viongozi wa kike, waliongoza na kuwasimamia watu katika dini ya Kikirsto. Miongoni mwao ni Esta ambae alikuwa Malkia na Debora alikuwa Nabii.

"Katika kanisa letu tumewachaguwa wanawake wawili   na wanaume wanne ambao  ni wachungaji na Wainjilist 12,  wanawake watano na wanaume saba, ndio wanaoongoza kanisa," alisema.

Mratibu  wa kuinua wanawake katika uongozi katika Chama Cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania  (TAMWA Zanzibar), Maryam  Ame, alisema wanatoa elimu  kwa wanawake wanaotaka  kuwa viongozi ili wajitambua na kutatua changamoto za kiuongozi.

Alisema  wanawake 172 Unguja na Pemba  wamepatiwa mafunzo ya uwongozi ambayo yamewasaidia kutambua vikwazo wanavyoweza kukutana navyo na namna ya kukabiliana navyo.

Aliwanasihi wanawake wanaotaka kuingia kwenye uongozi kutokuwa na hofu kwani hio ni haki yao iliyoainishwa katika katiba na mikataba mbali mbali ya kikanda na kmataifa ambayo nchi yetu imeiridhia na kuamua kuitekelkeza.


 

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.