JAJI MKUU ZANZIBAR ATAKA WANAFUNZI WA VYUO VYA MAFUNZO KUPATIWA ELIMU YA USHAURI NASAHA
NA FATMA HAMAD, PEMBA
Mahikimu wa mahakama za kadhi, Makamanda wa Vyuo vya mafunzo kisiwani Pemba wametakiwa kushirikia na Idara ya Msaada wa kisheria kuwapa elimu ya ushauri nasaha wanafunzi wa Vyuo vya mafunzo ili waweze kubadilika na kuwa na tabia njema.
Agizo hilo limetolewa na Jaji mkuu wa Zanzibar Ramadhan Khamis Abdala wakati akizungumza na wanafunzi pamoja na Makamanda wa Vyuo vya mafunzo kisiwani Pemba.
Alisema wengi wanaofikwa na mtihani wa kwenda kwenye vyuo vya mafunzo wanahisi kama wameonewa, hivyo ni vyema kuanzishwa utaratibu wa kupewa ushauri nasaha ili waweze kuondokana na mawazo hayo,na kuona watakaporudi katika familia zao wamebadilika tabia na kuwa Raia wema.
‘’Wenzetu hawa wanapokuja humu vyuoni huwa wanathirika kisaikologia, na kuhisi Serikali imewaonea hivyo ni budi kuwapa Mawaidha pamoja na ushauri nasaha ili ziweze kurudi akili zao, alisema.
Aidha alisema ni vyema kupatiwa misada midogo midogo ikiwemo Tende, hususan katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadani, kwani kutawafanya wafunge Ramadhani katika hali ya amani na utulivu licha ya kuwa hawako katika mikono ya familia zao.
Kwa upande wao wanafunzi wa vyuo vya mafunzo walisema changamoto kubwa inayowakwaza ni ucheleweshwaji wa kupata Prosija za kesi zao wakati wanapomba kwa ajili ya kukata rufa.
‘‘ kukata rufaa ni haki yetu hivyo mtu akiomba prosija apewe kwa haraka tunawaomba,walisema.
Aidha kwa upande mwengine waliitaka Serikali ya Mpinduzi Zanzibar kuongeza mahakimu wa Mahakama ya Rufaa kisiwani Pemba kwani kufanya hivyo kutapunguza wimbi kubwa la ucheleweshaji wa uwendeshaji wa kesi katika Mahakama hiyo.
‘’Kesi za Mahakama za Rufaa zinachelewa sana kwani kuwepo na mtendaji mmoja ni shida, tunaomba waengezwe tunakaa sana gerezani tunaumia,walieleza.
Nao viongozi wa vyio vya mafunzo walisema kitendo hicho kilichofanywa na Jaji mkuu na Timu yake kutembelea Vyuo vya mafunzo ni kitendo cha kupigwa mfano, kwani kutasaidia kutatuliwa kwa baadhi ya matatizo yanayowakumbwa wanafunzi vyuoni hapo.
Ziara hiyo ya kutembelea vyuo vya mafunzo ni utaratibu wa viongozi wa Mahakama kila ikikaribia siku ya sheria kuvitembelea vyuo vya mafunzo na kusikilizi kero za wanafunzi.
Comments
Post a Comment