NA SAID ABRAHMAN PEMBA.
NAIBU Katibu Mkuu wa
CCM Zanzibar Dkt, Abdalla Juma Sadalla (Mabodi) amelitaka jeshi la Kujenga
Uchumi Zanzibar (JKU) kujitoa na kutoa elimu Kwa wananchi juu ya kilimo Bora
ambacho kitaweza kuwaletea tija.
Alisema kuwa ni vyema
Kwa wataalamu wa kilimo wa jeshi hilo kutoa elimu zaidi Kwa wakulima ili tija
iweze kupatikana.
Mabodi aliyesema hayo
huko katika Viwanja vya maonesho ya siku chakula Duniani yanaendelea huko
Chamanangwe Wilaya ya Wete wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alieleza kuwa Jku ni
jeshi la Kujenga Uchumi hasa kwani limekuwa likifanya vizuri katika sekta ya
uzalishaji mali.
"Nina Imani kubwa
kuwa huko mbele ya safari Kuna hatari ya katika dhana ya Uchumi wa bluu kukawa
naushindani Mkubwa baina ya Jku na KM KM Kwa kiasi Fulani," alieleza
Mabodi.
Sambamba na hayo
Mabodi alifahamisha dhana nzima ya kuanzishwa Kwa Jku ni kutoa taaluma mbali
mbali Kwa Vijana wa kizanzibari ili waweze kujitegemea katika maisha yao na
kuacha kutegemea ajira kutoka Serikalini.
"Nilipongeze Jku
Kwa jitihada zake za kuweza kuwafundisha vijana wetu mbali mbali za stadi za
maisha,ukakamavu,uzakendo was nchi Yao,kwani asilimia kubwa ya Wananchi wetu ni
vijana," alisema Mabodi.
"Serikalini tuna
ajira ndogo na hivyo ni vigumu kusema kuwa wananchi wote waajiriwe, ninafahamu
hivi Sasa Kuna vijana wengi wanafunzwa ujasiriamali kupitia Jku,wengine
wanajifunza ufundi wa aina mbali mbali na wengine wanajinza mambo ya utalii na
ulinzi," alisema Mabodi.
Mapema naibu huyo
aliipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Kwa kutekeleza vyema ilani ya Chama Cha Mapinduzi Kwa
vitendo.
Maonesho ya siku ya
Chakula Duniani huadhimishwa kila ifikapo Octoba 10 ya kila mwaka ambapo
wananchi kutoka sehemu mbali mbali za Kisiwa Cha Pemba hupata fursa ya
kutembelea maeneo ya maonesho hayo yaliyopo Chamanangwe Wilaya ya Wete, Ujumbe
wa mwaka huu "Haachwi mtu nyuma,uzalishaji Bora,lishe Bora, mazingira Bora
na maisha Bora Kwa wote".
Comments
Post a Comment