WANDISHI WA HABARI WAPEWA MBINU.
FATMA HAMAD PEMBA.
Wandishi
wa habari Nchini wamekumbushwa kuitumia mitandao
ya kijamii kwa kuandika habari zenye ukweli na zenye
ubora ili kuepuka kuingia katika migoghoro isio
ya lazima.
Ukumbusho
huo umetolewa na Mwenyekiti wa Jumuia ya wandishi wa habari Pemba Pres Clab
[PPC] Bakar Mussa Juma wakati akizungumza na wandishi wa habari wa
mitandao katika mafunzo juu ya ulinzi na usalama wa mitandao ya kijamii
huko ofisi ya Ppc Chake chake Pemba.
Amesema
mitandao ya kijamii ndio chombo kinachofikisha ujumbe haraka kwa jamii hivyo ni
vyema kuwa makini wakati wanaporusha habari zao ili iweze kuwajenga na kuwa
huru katika kazi zenu.
Amesema
vyombo vya habari ndio sauti ya wasio na sauti hivyo sasa ni wakati
wa Wandishi kubadilika na waweze kuandika habari zenye
uhakika ambazo zitaleta tija kwa Jamii.
‘’Mitandao
ya kijamii ndio chombo kinachofikisha ujumbe kwa haraka katika jamii
hivyo lazima muwe makini sana katika kutumia hii mitandao kwani kumekua
na watu wakidukua habarinzenu mnazoziweka kwe mitandao’’ alisema katibu.
Aidha
katibu huyo amewahamasisha wandishi ambao bado hawajajiunga na
Clabu ya wandishi wa habari ili waweze kupata fursa mbali mbali za
kimaendeleo ambazo zimekua zikijitokeza clabuni hapo.
Mwenyekiti wa PPC Bakar Mussa Juma akizungumza na wandishi.
Mapema
mratibu wa Pemba Press Clab [PPC] Mgeni Kombo Khamis amewataka wandishi
waliopata mafunzo hayo kuyachukua na kuyafanyia kazi ili waweze kuandika vyema
habari zao.
Akitoa mafunzo mkufunzi wa mafunzo hayo Haji Nassor Mohad amewasisitiza wandishi hao kuifikisha taaluma hiyo kwa wandishi wenzao ili nawao wapate kunufaika na elimu hiyo.
Nao wandishi waliopata mafunzo hayo wameahidi kuyatumia vyema wakati wanapoandika habari zao jambo ambalo litasaidia kundika habari zisizo na migogoro.
Comments
Post a Comment