WAZAZI WAPEWA MBINU YA KUWALEA WATOTO WENYE ULEMAVU WA AKILI.
NA FATMA
HAMAD PEMBA 12/10/2022.
Wazazi na
walezi wanaoishi na watoto wenye ulemavu
wa akili wametakiwa kuzidisha ulinzi zaidi kwa watoto hao ili kuwalinda
na vitendo vya udhalilishaji.
Wito huo
umetolewa na mratibu wa jumuiya ya watu wenye ulemavu kisiwani Pemba [ZAPDD] Khalfan Amour Mohd wakati akizungumza na
wanachama wa jumuia ya watu wenye ulemavu wa akili huko Kiuyu mbuyuni wilaya ya
Micheweni mkoa wa Kasakazini Pemba kufuatia kuzuka kwa vitendo vya
udhalilishaji wanavyofanyiwa watu wenye ulemavu wa akili.
Alisema wapo watu
wamekua wakiwachukua watoto wenye ulemavu wa akili kwa ajili ya kumaliza haja zao za matamanio, hivyo wazazi
mnajukumu kubwa la kuhakikisha mnakuwa na ulinzi wa hali juu ili kuhakikisha
mda wote wapo katika hali ya amani na usalama vijana hao.
‘’Licha ya
halingumu mlizonazo za kimaisha lakini tuwashuhulikieni watoto wetu wenye
ulemavu tusiwabeze jamani’’ alisema mratib khalfan.
Kwa upande
wake msaidizi mwenyekiti wa jumuia ya
watu wenye ulemavu wa akili [ZAPDD] mkoa wa Kaskazi Pemba Zubeir Iddi
Khamis aliwataka wanajumuia hao kuvifichua
vitendo viovu wanavyofanyiwa watoto wenye ulemavu ikiwemo udhalilishaji
ili kufikishwa katika vyombo vya
kisheria.
Nae Mjumbe
kutoka Shijuwaza Aziza Alawi Mussa aliwashauri wazazi wanaoishi na watoto wenye
ulemavu kuziibua kero na changamoto zinazowakumba watoto hao kama vile
vibaskeli vya kutembelea ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.
‘’Tusiwadharau
watoto wetu wenye ulemavu huu ni mtihani mungu ametujalia ikiwa anashida ya Kigari,
Miwani toeni raarifa tunao wenzetu wa inclusive watatusaidia jamani’’
alifahamisha bi Aziza.
Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 15 kifungu kidogo cha kwanza kinasema kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na Nyumbani kwake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake.
Comments
Post a Comment