HIZI HAPA CHANGAMOTO WANAZOZIPATA WATU WENYE ULEMAVU.
Licha ya juhudi
zinazochukuliwa na Serikali pamoja na mashirika mbali mbali
yanayoshughulikia watu wenyeulemavu ili kuona watu wenye ulemavu wanaondokana na
vikwazo kadhaa, lakini bado wanaendelea kukubwa na matatizo mbali mbali ikiwemo ukosefu wa huduma.
Hayo
yamebainishwa na Mama mwenye
ulemavu wa viungo ambae pia ana
watoto 3 wenye ulemavu mchanganyiko
mkaazi wa Konde wilaya
ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba alisema bado anakabiliwa na changamoto ya upatikanaji pesa kwa ajili ya
kununulia huduma za watoto wake
hao.
Akizungumza
na mwandisi wa habari hizi huko
nyumbani kwake bi Asha Khamis Juma
mkazi wa Konde
kiungani mwenye ulemavu wa viungo
alisema bado anakabiliwa na changamoto
kubwa ya upatikanaji wa pesa kwa ajili ya kununulia
Pempasi pamoja na dawa.
‘’Kila siku
natumia elfu ishirini [20000] kwa ajili ya kununulia pempasi hivyo nateseka
sina uwezo nashinwa nahitaji msaada
jamani’’ alisema mama wa watoto wenye ulemavu.
‘’Mimi
mwenyewe kila baada ya mwaka mmoja na nusu nahitajika nitoe shilingi laki tano [5000,00] kwa ajili ya kununulia
mguu bandia, ukiangalia familia yangu ni masikini haiwezi kuhudumia gharama
zangu mimi pamoja na watoto wangu wenye
ulemavu’’ alieleza kwa masikitiko mama mwenye ulemavu.
Alifahamisha
kuwa kipindi cha nyuma Walikwenda watu wakampa msaada wa gari aina ya Keri kwa
ajili ya kuwapelekea watoto Hospital wakati watakapoumwa lakini haiwezi kuihudumia kwa sasa kutokana na hali
yake.
‘’Nilikuja nikapewa msaada wa keri lakini Hivi ninavyokuambia imelala bandani
haina mafuta na wale wahisani hawakuja tena’’ alisema mama.
Mapema Makamo mwenyekiti wa jumuia ya Wanawake wenye ulemavu Hidaya
Mjaka Ali aliwataka
wazazi wa watoto wenye ulemavu kuwafichua na kuwaunga katika jumuiya za watu wenye ulemau watoto hao
ili wapate kujulikana jambo
ambalo litasaidia kupata fursa mbali mbali za kimaendeleo wakati
zitakapotokezea.
Kwa mujibu
wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 12 [1] kinasema ‘’ Watu wote ni
sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote.
Comments
Post a Comment