WANAOFANYA MITIHANI WAONYWA


NA FATMA HAMAD PEMBA.

Wanafunzi wanaofanya mitihani ya Taifa wameonywa  kujiepusha na vitendo vya udanganyifu  wakati wakiwa katika mitihani yao ambavyo vitapelekea  kufutiwa  kwa  matokeo yao.

Nasaha hizo zimetolewa  na mbunge mstaafu wa jimbo la Kiwani Abdala Haji Ali katika hafla ya kuwaaga na kuwaombea duwa wanafunzi wanaofanya mitihani ya taifa  huko Skuli ya Chambani wilaya ya Mkoani mkoa wa Kusini Pemba.

Amesema nidhamu  ni moja ya sababu inayomfanya mwanafunzi kufanya vizuri hivyo ni vyema wawe na juhudu ya hali juu  kwenye masomo  ili muweze kuja kufaulu  mitihani yao.

,,Niwasihi watahiniwa  muwe na nidhamu ya hali ya juu msije mkakiuka sharia za mitihani kwani itakuja kuwa kulio kwenu’’ alisema mbunge mstaafu.


Kwa upande wake mwalimu mkuu skuli  ya  msingi  Said Faki Hassan amewataka wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma skulini hapo kuwa na mashirikiano ya pomoja kati yao na walimu kwani kufanya hivyo ndio msingi mkuu utakaosaidia kuleta maendeleo  na matokeo mazuri ya wananfunzi.


‘’Tuna masikitiko makubwa  wazee wa wanafunzi  bado hawako tayari kushirikiana na sisi pasi na kuwepo na nguvu zenu nyinyi hatuwezi kufika pahala tuijengeni chambani wazee huu si wakati wa kulaumiana,, alisema mwalimu mkuu.

Akisoma risala mwanafunzi wa skiuli hiyo mwanafunzi Ali Khamis amesema skuli yao inakabiliwa na changamoto mbali mbali  ikiwemo  uhaba  wa  walimu  wanaofundisha  masomo  ya  sayansi.

Nae mwalimu msimamizi wa Serikali ya wanafunzi Chambani Khamis Othman amesema imekua ni kawaida yao kila mwaka kufanya hafla hiyo ya kuwaombea dua wanamitihani wa darasa la

kumi na mbili, la kumi, la saba na darasa la Nne.


Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.