MKUU WA MKOA AIPA TANO JKU


                      NA SAID ABRAHMAN PEMBA.

MKUU wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa amesifu mbinu zinazochukuliwa na Jku za utumiaji wa eneo dogo la uzalishaji Kwa kupata mazao mengi 

 Alieleza kuwa Tanzania Bara wamekuwa wakitumia ardhi kubwa Kwa Kilimo huku rasilimali wanazotumia ni kidogo.

 Mkuu huyo wa Mkoa aliyasema hayo Chamanangwe Wilaya ya Wete, wakati alipokuwa akiangalia shughuli mbali mbali zinazofanya na Jku, kwenye maonesho ya siku ya chakula Duniani yanayoendelea huko.

 Fatma alisema kuwa amefarajika sana kuona utaalamu ambao unafanywa na Jku wa kutumia  ardhi ndogo katika shughuli za Kilimo Kwa kupanda mazao mchanganyiko huku mavuno yake yakiwa mengi.

 "Nimefarajika sana kuona kumbe mkulima anaweza kulima sehemu ndogo tu lakini mavuno yake yakiwa  ni mengi, Kwani sisi kule kwetu tumekuwa tukilima maeneo makubwa na wakati mwengine mavuno yanakuwa hafifu," alisema Fatma.

 Nae Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Yussuf Ali aliwataka vijana kujiunga na Jku Kwa lengo la kujikomboa kimaisha na kiutamaduni.

 Alisema kuwa Jku imekuwa ikitoa taaluma mbali mbali za ujasiriamali Kwa wananchi tofauti, hivyo aliwataka vijana kunitumia fursa hiyo ili waweze kujifunza mambo mengi ambayo yataweza kuwasaidia katika maisha yao.

 "Niwaombe vijana wote ambao hawajajiunga na JKU wajiunge na jeshi hili kwani Kuna fursa nyingi ambazo zinatolewa na wenzitu wa Jku," aisema  Yussuf.

  "Jku imekuwa ikiwaendeleza vijana wengi hasa wale ambao wanamaliza darasa la kumi (f11) au (fIV) kwani wamekuwa wakitoa elimu ya ujasiriamali Kwa wananchi wote," alisema Yussuf.

 Sambamba na hayo Mwenyekiti huyo aliwafahamisha wananchi kuwa Jku ni chombo Chao, hivyo aliwasisitiza wazazi kuwapeleka vijana wao Jku ili waweze kupata taaluma ambazo zinatolewa huko.

 Mapema Yussuf aliwataka wananchi kutembelea katika mabanda ya Jku Chamanangwe Ili kujionea wenyewe lakini pia kupata taaluma.

 "Niwanasihi wananchi kuwa maonesho haya ni Bure, hivyo ni vyema wafike Kwa wingi Kwa ajili ya kujifunza mambo mbali mbali ambayo yatawasaidia katika maeneo yao," alisema Yussuf.

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.