WANANCHI WANAOISHI KATIKA NYUMBA ZA MAENDELEO WAHIMIZWA USAFI

NA SAID ABRAHMAN PEMBA.

 SHIRIKA la nyumba Kisiwani Pemba limewataka wananchi wanaoishi katika nyumba za maendeleo zilizopo Mtemani Wete kushirikiana pamoja katika suala Zima la Usafi katika maeneo yao .

Hayo yalielezwa na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la nyumba na makaazi Kisiwani Pemba Ali Mgau wakati alipokuwa akizungumza na wakaazi wa nyumba namba 5 huko Mtemani Wete.

Alieleza kuwa kuanzia Sasa Shirika limeamua kuwashirika na wananchi wanaoishi katika nyumba hizo katika matengenezo hasa uzibuaji na utapishaji wa Makaro ambayo yameshajaa au kuziba.

"Kuanzia Sasa Shirika letu limeamua kuwaachia wananchi wenyewe suala la uzibuaji au utapishaji wa Makaro,Shirika litasaidia pale ambapo litahitajika kufanya hivyo," alieleza Mkurugenzi Mgau.

Sambamba na hayo Kaimu huyo aliwataka wakaazi hao ambao mikataba yao imemalizika kufika ofisini kwao ili kujaza mikataba mengine mipya.

"Hivi Sasa Tunataka kufanya uhakiki wa wapangaji wetu ambao wanakaa katika majumba haya ya maendeleo, hivyo Kwa wale ambao mikataba yao imemalizika kufuata taratibu za kujaza mikataba mengine," alifahamisha Kaimu Mkurugenzi.

Akizungumzia suala la ukarabati wa majumba hayo, Kaimu huyo alieleza kuwa Kwa Sasa Shirika la nyumba limeelekeza nguvu zake zote katika majumba ya Wete na kuanzia wataanza na jumba namba 4 na kuendelea namba 5.

"Baada ya kumaliza kuyafanyia ukarabati majumba ya maendeleo ya Madungu Chake Chake, tumeona ni vyema kuendelea kuyakarabati majumba ya Wete kwanza na baadae tutaendelea na kazi hiyo Kwa upande wa Mkoani,' alisema Mgau.

Ama Kwa ulipaji wa Kodi, Kaimu Mgau alieleza kuwa hivi sasa wanatakiwa kulipa zao Kwa kutumia njia sahihi iliyokwa na Serikali.

"Kwa Sasa Shirika limekuwa na mfumo mpya wa ulipaji wa Kodi Kwa kutumia njia "system ", hivyowananchi tulipeni Kodi zetu na pale ambapo patakuwa na kasoro ni vyema kufika ofisini kwetu ili kuweza kupata muongozo," alisema Mgau.

"Lakini niwashauri wananchi ambao mnaoishi katika nyumba namba 5, azisheni kamati yenu ambayo itaweza kusimamia suala Zima la Usafi katika maeneo yenu, pale ambapo patatokea hitilafu kamati iweze kufanikisha tatizo hilo," alisema Mgau.

Nae afisa Utumishi kutoka Shirika la nyumba Pemba Mohammed Juma aliwapongeza wananchi hao Kwa kujitahidi kuweka Usafi katika maeneo yao.

Aidha aliwasisitiza wakaazi hao kuendelea kulipa Kodi zao Kwa wakati kwani fedha ambazo wanazozilipia Kodi ndio zinazotumika katika kuendeshea ukarabati wa majengo hayo.

Nae Sheha wa Shehia ya Mtemani Mrisho Juma Mtwana aliwataka wakaazi hao kuendelea kushirikiana pamoja na uongozi wa Shirika la nyumba Kwa kuondoa changamoto zilizopo.

Aidha Sheha huyo aliwasisitiza wakaazi hao kuwa kitu kimoja pale wanapopanga Mipango yao ya maendeleo katika Shehia yao iweze kufanikiwa.

Nao wakaazi wa nyumba hizo wamelipongeza Shirika la nyumba Pemba Kwa mashirikiano yao na kulitaka kuendelea kushirikiana nao kwa kila Hali.

Othman Mcha Ramadhan aliliomba Shirika la nyumba kubeba gharama za ujenzi wa karo ambalo tayari limeziba kutokana na Hali ya maisha ilivyo.

"Kwa vile hili ni kwanza kwetu, tunaliomba Shirika libebe gharama zote za usafishaji wa hili karo na litapitokezea jengine gharama tutabeba sisi wenyewe," alisema Othman .

Nae Salum Said Shaame alieleza kuwa mara nyingi kunapotokezea tatizo katika nyumba zao au kuziba Kwa chemba za vyoo hulazimika kutoa fedha zao na kuwalipa mafundi wanaofanya Kazi bila ya kushirikisha Shirika .

"Kiufupi pale ambapo kumetokezea tatizo ikiwa ni ndani ya nyumba au kwenye chemba zetu mafundihuwa tunawalipa sisi wenyewe bila ya msaada kutoka Shirika," alieleza Salum.


Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.