MUHALI BADO NI TATIZO.
NA FATMA
HAMAD PEMBA.
Jamii
imekumbushwa kujitokeza kwa wingi mahakamani kutoa ushahidi kwa kesi za udhalilishaji jambo ambalo
litasaidia wahalifu wa makosa
hayo kutiwa hatiani na kupata hukumu.
Ukumbusho
huo umetolewa na Hakimu wa mahakama aneshughulikia kesi za udhalilishaji Mkoa wa Kusini Pemba Muumin Ali Juma wakati akizungumza na mwandishi wa habari
hizi huko ofisini kwake amesema licha ya
Serikali ya Mapinduzi kuweka mikakati mbali mbali ili kuondosha makosa hayo, ikiwemo uwepo wa mahakama maalumu lakini bado
wananchi hawajataka kutoa ushirikiano juu ya mahakama hiyo.
Amesema
wananchi waliowengi hawataki kusimama mahakamani kutoa ushahidi na badala
yake huyakalia kitako na kuyafanyia
suluhu matukio ya udhalilishaji wakati yanapotokezea katika familia zao hali ambayo inasababisha kesi nyingi kufutwa
mahamani kutokana na kukosa ushahidi.
‘’ kwa
kweli tunakilio kikubwa Jamii
wenyewe hawajataka kuyaondosha matendo ya udhalilishaji’’ alisema hakimu
Muumin.
Alifafanua
kuwa kesi nyingi ambazo hazitiwi hatiani na kupata hukumu ni za watoto kuanzia
miaka 15 hadi 17.
Alieleza
kuwa kila mmoja kwa nafasi yake aweze
kuumwa na vitendo vya udhalilishaji na kuweza kuchukua hatua kwani kumbuka leo kafanyiwa mtoto wa mwenzako
kesho huenda akafanyiwa wa kwako.
Kwa
upandewake Fatma Rashid Abdala mwanaharakati wa kupinga masuala ya
udhalilishaji kutoka shehia ya Sizini alisema nivyema kwa Serikali kuwachukulia
hatua kali za kisheria kwa wale wote wanaokataa kutoa ushahidi ili iwe muarubaini wa hilo.
Nae mratibu wa chama cha wandishi wa habari
wanawake Tanzania Tamwa Fathiya
Mussa Said amesema wakati umefika
kwa wananchi kuacha muhali juu ya
masauala ya udhalilishaji.
Jumla ya
mashauri 37 ya udhalilishaji
yamepokelewa mahakamani hapo tokea
kuanzishwa mahakama maalumu kwa mwaka huu wa 2022, ambapo mashauri 32 yalirithiwa kutoka mahakama mchanganyiko,
mashauri 42 tayari yameshatolewa mamuzi kati ya hayo 7 ndio yaliopata hatia, yaliobakia yalifutwa
kutokana na kukosa ushahidi.
Comments
Post a Comment