HALMASHAURI NA MABARAZA YA MIJI YAHIMIZWA USHIRIKIANO.

                                     NA SAID ABRAHMAN PEMBA. 12/10/2022

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Massoud Ali Mohammed  aliwataka  watendaji  wa  halmashauri  ya Micheweni, baraza la Mji Wete pamoja na Madiwani kuwa na mashirikiano katika utendaji wao kazi za kila Siku . 

 Alisema kuwa hakuna miujiza yeyote ambayo inayoweza kutokezea wakati watendaji hao wakiwa hawana ushirikiano nzuri katika majukumu yao.

 Waziri Massoud aliyesema hayo huko katika Ukumbi wa Jamhuri hall Wete wakati akizungumza na watendaji hao na kuwaeleza kuwa mashirikiano ndio kitu pekee ambacho kitawafanya kuwa na Ari, umoja na moyo wa kufanya kazi.

 Alifahamisha kuwa kumekuwa na baadhi ya watendaji kutoka katika mabaraza ya miji,halmashauri au hata Madiwani kuweka vikwazo katika miradi ya maendeleo Kwa madai tu mrado huo umepelekwa na mtu Fulani na hivyo kuuwekea pingamizi jambo ambalo sio sahihi hata kidogo.

 "Moja ya changamoto ambayo iko Serikali zetu za Mitaa ni kukosekana Kwa mashirikiano ya dhati Kwa baadhi ya watendaji jambo ambalo linadhoofisha utendaji wa taasisi hizo katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila Siku," alisema Waziri Massoud.

 Massoud aliwaeleza watendaji hao kuwa kazi yao kubwa ni kuwatatulia wananchi changamoto zao na Wala sio kuwazidishia shida katika maeneo yao.

 "Niwaombe wakuu wa Wilaya ya Wete na Micheweni kufuatilia Kwa ukaribu sana mijadala au shughuli zinazofanywa hasa za miradi ndani ya Serikali za Mitaa inakwenda vipii,"alisema Waziri.

 "Na hapa ninachotaka kufuatiliwa zaidi ni kile ambacho kinaanzishwa kiweze kumalizika na kutumika Kwa wananchi wetu," alifahamisha Massoud.

 Akizungumzia suala la utoaji wa ujenzi wa wananchi,Waziri huyo alisema Yuko tayari kumsimamisha kazi au kumfukuza mtendaji yeyote ambae ataweza kutoa kibali Cha ujenzi bila ya kufuata taratibu zilizopo.

 Alisema kuwa Kuna baadhi ya watendaji ambao wamepewa jukumu la utoaji wa vibaji vya ujenzi Kwa wananchi lakini hawaangalii vigezo vya ujenzi huo.

 "Endapo itatokezea mtendaji yeyote akatoa kibali na baada ya kukitoa pakaonekana sehemu hiyo Ina mgogoro na mwananchi huyo kutakiwa kuvunja, kabla ya kuvunjwa sehemu hiyo mtendaji wewe nitakufuta kazi mara moja," alisema Waziri Massoud.

 Hata hivyo Massoud aliwaomba Madiwani kutojiingiza katika masuala ya migogoro ya ardhi kwa namba yeyote ile.

.Mapema Waziri Massoud aliwaeleza watendaji hao kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ inatambua uwepo wao pamoja na kuuthamini kazi wanazozifanya za kuleta maendeleo katika jamii 

 Nae Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni  Khatib   Yahya alimuhakikishia Waziri huyo kuwa maangizo yote pamoja na ushauri ambao aliwapatia watayafanyia kazi Kwa kushirikiana Kwa pamoja.

 Aidha Mgeni alimpongeza Waziri huyo Kwa mashirikiano anayowapa na kumtaka kuendelea kuwa nao karibu Kwa kila Hali .

 "Lakini pia tunampongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Hassan Mwinyi kwa juhudi zake anazozitoa Kwa wananchi wetu," alisema Mgeni.

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.