NA SAID ABRAHMAN PEMBA. 12/10/2022
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za
Mitaa na Idara Maalum za SMZ Massoud Ali Mohammed aliwataka watendaji wa halmashauri ya Micheweni, baraza la Mji Wete pamoja na
Madiwani kuwa na mashirikiano katika utendaji wao kazi za kila Siku .
Alisema kuwa hakuna
miujiza yeyote ambayo inayoweza kutokezea wakati watendaji hao wakiwa hawana
ushirikiano nzuri katika majukumu yao.
Waziri Massoud
aliyesema hayo huko katika Ukumbi wa Jamhuri hall Wete wakati akizungumza na
watendaji hao na kuwaeleza kuwa mashirikiano ndio kitu pekee ambacho
kitawafanya kuwa na Ari, umoja na moyo wa kufanya kazi.
Alifahamisha kuwa
kumekuwa na baadhi ya watendaji kutoka katika mabaraza ya miji,halmashauri au
hata Madiwani kuweka vikwazo katika miradi ya maendeleo Kwa madai tu mrado huo
umepelekwa na mtu Fulani na hivyo kuuwekea pingamizi jambo ambalo sio sahihi
hata kidogo.
"Moja ya
changamoto ambayo iko Serikali zetu za Mitaa ni kukosekana Kwa mashirikiano ya
dhati Kwa baadhi ya watendaji jambo ambalo linadhoofisha utendaji wa taasisi
hizo katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila Siku," alisema Waziri
Massoud.
Massoud aliwaeleza
watendaji hao kuwa kazi yao kubwa ni kuwatatulia wananchi changamoto zao na
Wala sio kuwazidishia shida katika maeneo yao.
"Niwaombe wakuu
wa Wilaya ya Wete na Micheweni kufuatilia Kwa ukaribu sana mijadala au shughuli
zinazofanywa hasa za miradi ndani ya Serikali za Mitaa inakwenda
vipii,"alisema Waziri.
"Na hapa
ninachotaka kufuatiliwa zaidi ni kile ambacho kinaanzishwa kiweze kumalizika na
kutumika Kwa wananchi wetu," alifahamisha Massoud.
Akizungumzia suala la
utoaji wa ujenzi wa wananchi,Waziri huyo alisema Yuko tayari kumsimamisha kazi
au kumfukuza mtendaji yeyote ambae ataweza kutoa kibali Cha ujenzi bila ya
kufuata taratibu zilizopo.
Alisema kuwa Kuna
baadhi ya watendaji ambao wamepewa jukumu la utoaji wa vibaji vya ujenzi Kwa
wananchi lakini hawaangalii vigezo vya ujenzi huo.
"Endapo itatokezea
mtendaji yeyote akatoa kibali na baada ya kukitoa pakaonekana sehemu hiyo Ina
mgogoro na mwananchi huyo kutakiwa kuvunja, kabla ya kuvunjwa sehemu hiyo
mtendaji wewe nitakufuta kazi mara moja," alisema Waziri Massoud.
Hata hivyo Massoud
aliwaomba Madiwani kutojiingiza katika masuala ya migogoro ya ardhi kwa namba
yeyote ile.
.Mapema Waziri Massoud
aliwaeleza watendaji hao kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Ofisi
ya Rais, Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ inatambua uwepo
wao pamoja na kuuthamini kazi wanazozifanya za kuleta maendeleo katika
jamii
Nae Mkuu wa Wilaya ya
Micheweni Mgeni Khatib Yahya alimuhakikishia Waziri huyo kuwa maangizo yote
pamoja na ushauri ambao aliwapatia watayafanyia kazi Kwa kushirikiana Kwa pamoja.
Aidha Mgeni
alimpongeza Waziri huyo Kwa mashirikiano anayowapa na kumtaka kuendelea kuwa
nao karibu Kwa kila Hali .
"Lakini pia
tunampongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein
Ali Hassan Mwinyi kwa juhudi zake anazozitoa Kwa wananchi wetu," alisema
Mgeni.
Comments
Post a Comment