wandishi wa habari wahimizwa kuandika habari za watu wenye ulemavu
NA FATMA
HAMAD PEMBA 8/3/ 2022.
Wandishi wa
habari wametakiwa kujikita zaid maeneo ya Vijijini ili kuibua kero na changamoto ambazo
zimekuwa zikiwakumba watu wenye ulemavu.
Wito huo
umetolewa na Waziri wanchi ofisi ya makamo wa kwanza wa rais Zanzibar Saada
Mkuya Salim wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wandishi wa habari wa
vyombo mbali mbali Zanzibar huko ukumbe wa Maru maru Hoteli kisiwani
unguja.
Alisema watu wenyeulemavu wamekuwa wakikumbana na
matatizo mbali mbali hivyo ni wakati wandishi kujitoa na kuzibua kero ili ziweze kufikia kwa jamii na kupatiwa
ufumbuzi.
‘’Nyinyi
wandishi wa habari mnamchango mkubwa wa
kubadilisha maisha ya watu wenye ulemavu hivyo msikae tu bali nendeni
mkaibuwe na muweze kuyatoa katika vyombo
vya habari jambo ambalo litamfanya kila aneguswa na hilo aweze kutimiza
majukumu yake kwa mujibu wa nafasi yake alionayo’’ alieleza waziri.
Kwa upande
mwengine waziri sada aliwasihi wazazi ambao wana watoto wenye ulemavu kuacha
tabia ya kuwafungia ndani watoto hao kwani nawao wanahaki ya kupata mahitaji
mbali mbali ikiwemo Elimu na Uongozi kama watoto wengine.
Mapema mkuu wa program kutoka shirika la Internews
Tanzania Shaban Maganga alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na
kuwapatia mbinu mbadala ambazo
zitawawezesha kuandika na kuripoti
habari za watu wenye ulemavu jambo ambalo litaleta mabadiliko kwa watu hao.
Nae Mkuu
wa mradi mjumuishi wa Vyombo vya Habari
kanda ya Afrika Jackie lidubwi amewataka waandishi wa Habari kuwashirikisha
watu wenye ulemavu kwa kuwapa nafasi za kueleza shida zao wakati wanapoandika
habari zao.
Aidha
aliwashauri wandishi wa habari kutumia majina sahihi wakati wanapoandika na
kuripoti habari za watu wenye ulemavu ambayo hayataleta athari kwa watu hao
katika jamii.
Baadhi ya
wandishi walioshiriki mkutano huo wamewataka watendaji wa Internews kuendelea
kutoa mafunzo mbali mbali ikiwemo ya
lugha za alama jambo ambalo litawazesha wandishi hao
kuzungumza na kuibua kero za watu wenye ulemavu wa aina zote.
Mafunzo hayo
ya siku mbili yaliyoshirikisha waandishi kutoka Unguja na Pemba yamelenga
kuongeza uwelewa kwa waandishi wa Habari katika kuripoti habari zinazohusu watu
wenye ulemavu Visiwani Zanzibar.
Comments
Post a Comment